Pata taarifa kuu
MAREKANI-KENYA-DIPLOMASIA-USALAMA-UGAIDI

Marekani yawaonya raia wake kutotembelea Kenya hivi karibuni

Nchi ya Marekani imewaonya raia wake walioko nchini Kenya na wale wanaopanga kusafiri kuelekea nchini humo siku chache kabla ya rais Barack Obama kuzuru nchi hiyo kwa kile Marekani inachodai ni kuwepo kwa tishio la shambulio la kigaidi.

Rais wa Marekani, Barack Obama, akijianda kufanya ziara ya kikazi nchini Kenya.
Rais wa Marekani, Barack Obama, akijianda kufanya ziara ya kikazi nchini Kenya. REUTERS/Andrew Harnik/Pool
Matangazo ya kibiashara

Wizara ya mambo ya nje ya Marekani kwenye taarifa yake, imesema kuwa kutokana na ukweli kwamba kutakuwa na mkusanyiko mkubwa wa watu, makundi ya kihalifu hupendelea kutumia mwanya huo kuwalenga washiriki na wageni wengine.

Tangazo hili limewaonya raia wake kuhusu kukaa kwenye mikusanyiko ya watu wakati wa ziara hiyo au hata kabla na kuwataka kuwa katika hali ya tahadhari muda wote wawapo nchini humo kufuatia taarifa za kiintelijensia kuwa huenda magaidi wakatekeleza shambulio.

Onyo hili la Marekani linatolwa wakatu huu nchi ya Kenya ikiendelea kushuhudia mashambulizi kadhaa ya kigaidi yanayotekelezwa na wapiganaji wa kundi la Al-Shabab nchini Somalia, ambapo mwezi april mwaka huu kundi hilo lilitekeleza mauaji ya watu 148 katika Chuo kikuu cha Garisa kaskazini mwa nchi hiyo.

Ziara ya rais Obama nchini Kenya itakuwa ni ziara yake ya nne katika bara la Afrika toka alipokuwa rais wa Marekani na ni ziara ya kwanza kuifanya nchini humo toka alipochukua madaraka mwaka 2009.

Ziara hii inachukuliwa kwa umakini mkubwa na wananchi wa Kenya kwa kile ambacho wanadai kuwa kiongozi huyo ana mizizi nchini humo kwa kuwa baba yake mzazi ana asili ya Kenya. Rais Obama atahutubiwa mkutano wa kimataifa kuhusu ujasiriamali July 24 mwaka huu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.