Pata taarifa kuu
BURUNDI-EAC-USALAMA-SIASA

Burundi: Yoweri Museveni atangaza "mazungumzo mapya"

Kufuatia mashauriano na pande zote nchini Burundi, mpatanishi wa Umoja wa Afrika akiwa pia rais wa Uganda, Yoweri Kaguta Museveni, ametangaza kuwa mazungumzo mapya yatafanyika ili kumaliza mgogoro unaoendelea Burundi.

Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni wakati alipokua akiendesha vikao mbalimbali mjini Bujumbura, Jumatano Julai 15.
Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni wakati alipokua akiendesha vikao mbalimbali mjini Bujumbura, Jumatano Julai 15.
Matangazo ya kibiashara

Yoweri Kaguta Museveni anatazamiwa kumtuma Ijumaa wiki hii na mpaka mwisho wa mazungumzo waziri wake wa Ulinzi.

Baada ya miezi kadhaa ya mgogoro, na ikiwa imesalia wiki moja ya uchaguzi wa rais ambao umepangwa kufanyika Julai 21, rais wa Uganda alikutana Jumatano wiki hii na pande husika ili kujaribu kutafutia ufumbuzi mzozo huo.

Yoweri Museveni ambaye ameteuliwa kuwa msuluhishi wa Umoja wa afrika katika mzozo huo unaoshuhudiwa Burundi, amekutana Jumatano wiki hii na wajumbe wa chama tawala, lakini mazungumzo yanaonekana kufanyika kwa mwendo wa kinyonga.

Ndani ya wiki moja, tarehe 21 Julai, utakaofanyika uchaguzi wa urais ambao unatia wasiwasi jumuiya ya kimataifa, baada ya miezi ya mgogoro kufuatia muhula wa wtatu wa rais Pierre Nkurunziza. Msuluhishi wa Umoja wa Afrika Yoweri Museveni aliwasili Jumanne wiki hii katika mji wa Bujumbura, anaendelea na mikutano yake na pande husika katika mzozo huo.

Adhuhuri, rais wa Uganda amekutana kwa mara ya pili katika siku ya leo Jumatano, na kambi ya rais. Mkutano wa kwanza kati ya Yoweri Museveni na wawakilishi wa chama tawala cha Cndd-Fdd, serikali na wajumbe wa Ofisi ya rais, ulikua umefanyika asubuhi Jumatano wiki hii. Wawakilishi wa kambi ya rais, hata hivyo, wameomba kikao kiahirishwa , ili waweze kwanza kukutana baina yao.

Wakati wa kipindi cha mapumziko hayo, rais wa Uganda amekutana na marais wa zamani nchi ya Burundi ili aweze kusikia maoni yao juu ya mgogoro unaoendelea nchini humo. vikao hivyo ambavyo inaonekana kwamba ni vigumu kupata ufumbuzi katika muda wa saa chache kabla ya kuondoka nchini kwa mpatanishi.

Upinzani, na vyama vya kiraia wamebaini kwamba wana matumaini kuwa huenda mazungumzo hayo yakaleta muafaka, kutokana na jinsi yalivyoanza, na jinsi rais Museveni alivyosikiliza hoja za kila pande.

Leo, rais wa Uganda inaonekana kuwa ameondoka nchini akiwa na wazo la kuzindua mazungumzo haya na waziri wake wa ulinzi, ambaye atajielekeza mjini Bujumbura kukutana na pande zote na kujaribu kuendeleza faili hiyo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.