Pata taarifa kuu
MISRI-SHERIA

Rais wa Misri aahidi kuwaadhibu washukiwa wa ugaidi

Rais wa Misri Abdel Fatah al-Sisi ameahidi hii leo kutumia sheria ngumu dhidi ya ugaidi, ikiw ani siku moja baada ya kutokea kwa mauaji ya hakimu mkuu wa jamahuri aliaupoteza maisha katika shambulio la kujitoa muhanga.

rais wa Misri Abdel Fattah al-Sisi
rais wa Misri Abdel Fattah al-Sisi REUTERS/Amr Abdallah Dalsh
Matangazo ya kibiashara

Katika hotuba yake iliotolewa wakati wa mazishi ya hakimu Hacham Barakat, na ambayo ilipeperushwa moja kwa moja kwenye kituo cha runinga ya taifa, al-Sisi amesema watafanya mageuzi ya sheria hara iwezekanavyo bila kuchelewa ili kutoa adhabu kali dhidi ya magaidi.

Jana jumatatu hakimu mkuu wa jamuhuri alipoteza maisha wakati akipelekwa Hospitalini baada ya msafara wake kushambuliwa kwa bomu katika mji wa kitajiri nchini humo.

Tangu pale al-Sisi kiongozi wa jeshi alipompindua rais Mohamed Morsi Julay 2013, makundi ya kigaidi yameongeza kasi yamashambulizi ya hapa na pale yakilenga vikosi vya Usalama wakidai kulipia kisase dhidi ya wafuasi wa rais aliepinduliwa ambao wengi walipoteza maisha wakati wa kuzima maandamano ya kupinga mapinduzi ya kijeshi huku wengine wakiendelea kufanyiwa vitisho na vitimbi na wengine wakizuiliwa jela.

Hicham Barakat aliekuwa na umri wa miaka 64 alikuwa ni kiongozi mkuu wa serikali ambae alikuwa ana shikilia sheria ameuawa katika mlolongo wa mauaji ya kuvizia yanayoendelea nchini humo.

Zaidi ya watu 1.400 waliokuwa wanazuiliwa wakiwemo wafuasi wa chama cha kiislam waliauwa katika vurugu huku wengine mamia wakitiwa nguvuni. Mamia tayari wamehukumiwa adhabu ya kifo inayopingwa na Umoja wa Mataifa UN lakini pia mahakama ya kikatiba ambayo imetupilia mbali hukumu kadhaa na kuomba kesi kusikilizwa tena upya.

Al Sisi amesema hawatosubiri miaka 5, 10 ili kuwahukumu watu wanaouwa wengine, iwapo itatokea hukumu ya kifo, itatekelezwa mara moja, kabla ya kusisitiza neno Sheria, Sheria, sheria.

Tangu mwaka 2013 mashambulizi ya kijihadi dhidi ya vikosi vya Usalama yanaripotiwa katika eneo la kaskazini mwa Sinai. Kundi lenye uhusinao na kundi linalojiita Islamic State ndilo lililojigamba kuhusika katika shambulio baya kuwahi kushuhudiwa nchini humo.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.