Pata taarifa kuu
BURUNDI-UCHAGUZI

Zoezi la upigaji kura laanza nchini Burundi

Vituo vya kupigia kura vimeanza kufunguliwa katika baadhi ya maeneo nchini Burundi ambapo kumeripotiwa mashambulizi katika vituo kadhaa, mashambulizi ambayo yanaelezwa hayakuathiri lolote kuhusu vifaa vya kupigia kura.

Wafanyakazi wa tume huru waliokuwa wakiandaa vifaa kwa ajili ya Uchaguzi
Wafanyakazi wa tume huru waliokuwa wakiandaa vifaa kwa ajili ya Uchaguzi REUTERS/Paulo Nunes dos Santos
Matangazo ya kibiashara

Uchguzi huo unafanyika licha ya shinikizo la Jumuiya ya Kimataifa kuitaka serikali ya Burundi kutaka kuahirishwa kwake na kupanga kalenda nyingine inayo kubalika na pande zote husika na chaguzi nchini humo.

Upinzani nchini humo ulitangaza kususia katika kilichodaiwa kuwa hauwezi kuwa huru na haki.

Hayo yanajiri wakati kambi ya rais Nkurunziza ikiendelea kupata pigo kubwa kutoka na baadhi ya wajumbe kuendelea kujiondowa na kukimbilia uhamishoni ambapo hapo jana spika wa bunge la nchi hiyo Pie Ntavyohanyuma alitangaza kuitoroka nchi na kukimbilia uhamishoni.

Akizungumza akiwa jijini Brussels nchini Ubelgiji, spika wa Bunge Pie Ntavyohanyuma amemtolea wito rais Nkurunziza kurejelea upya mpango wake wa kuwania urais katika uchaguzi wa Julay 15.

hii inakuja baada ya makam wa pili wa rais Gervais Rufyikiri kutangaza pia kutoroka nchi kama vile wajumbe wengine wa chama tawala cha CNDD-FDD kutokana na vitisho kuhusu msimamo wao wa kutounga mkono muhula wa tatu wa rais Nkurunziza.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.