Pata taarifa kuu
BURUNDI-POLISI-WANAFUNZI

Burundi: mamia ya wanafunzi waingia katika Ubalozi wa Marekani

Wanafunzi 200 wa Chuo kikuu cha taifa nchini Burundi wameingia katika majengo ya ubalozi wa Marekani mjini Bujumbura kuomba hifadhi, baada ya kuvamiwa na askari polisi katika eneo walipokua wakipiga kambi.

Mjini Bujumbura, wanafunzi 200 wa Chuo kikuu cha taifa wameingia katika majengo ya ubalozi wa Marekani kuomba hifadhi, Juni 25 mwaka 2015.
Mjini Bujumbura, wanafunzi 200 wa Chuo kikuu cha taifa wameingia katika majengo ya ubalozi wa Marekani kuomba hifadhi, Juni 25 mwaka 2015. AFP PHOTO/MARCO LONGARI
Matangazo ya kibiashara

Wanafunzi hao wamekua wakipiga kambi tangu mwishoni mwa mwezi Aprili mbele ya ubalozi wa Marekani, ambapo walikua wakiomba ulinzi baada ya kufukuzwa katika mabweni yao wakati yalipoanza maandamano dhidi ya muhula wa tatu wa rais Nkurunziza.

Mpaka leo Alhamisi, wanafunzi 200 wa Chuo kikuu cha taifa ndio wamekua wakipiga kambi nje ya ubalozi wa Marekani mjini Bujumbura. Chuo hiki cha taifa kilifungwa na viongozi wa Burundi Aprili 30 wakati ambapo wanafunzi waliituhumiwa kuwa miongoni mwa waandamanaji wanaopinga muhula wa tatu wa rais Pierre Nkurunziza. Tangu wakati huo wanafunzi hao wamekua wakipiga kambi nje ya ubalozi wa Marekani mjini Bujumbura.

Alhamisi wiki hii, polisi ilijaribu bila mafanikio kuwaondoa wanafunzi hao kwenye eneo hilo. Polisi ilikua imejiandaa kwa kutumia nguvu ili kuwaondoa wanafunzi hao. Wakati ambapo polisi ilijaribu kuwasogelea, wanafunzi hao walikusanyika kwenye mlango wa kuingilia na kupanda mlango huo kwa muda mcamche sana.

Baadhi wamepita juu ya mlango, wengine chini. Kwa sasa wanafunzi wote wameingia katika majengo ya ubalozi wa Marekani, na wanapatikana wakati huu katika eneo ambapo magari yanakoegeshea, eneo ambapo polisi haiwezi kuwafikia.

Juu ya paa za majengo ya ubalozi, kikosi cha majini cha Marekani kimeweka ngome zake. Na nje ya ubalozi huo, askari polisi wa Burundi wamevunja kambi ya muda iliyojengwa na wanafunzi hao. Polisi imeonekana ikipakia ndani ya gari, magodoro, masanduku na vitu vingine ambavyo viliachwa na wanafunzi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.