Pata taarifa kuu
BURUNDI-MAANDAMANO-USALAMA-SIASA

Aprodh: " machafuko yasababisha vifo vya watu 70 Burundi "

Mpaka sasa idadi kamili ya watu waliouawa nchini Burundi imekua bado haijatolewa, baada ya mwezi moja na nusu wa maandamano dhidi ya muhula wa tatu wa rais Pierre Nkurunziza.

Maandamano kujeruhiwa, alikamatwa na polisi wakati wa mapigano tarehe 27 Aprili.
Maandamano kujeruhiwa, alikamatwa na polisi wakati wa mapigano tarehe 27 Aprili. REUTERS/Thomas Mukoya
Matangazo ya kibiashara

Shirika la haki za binadamu na za wafungwa Aprodh, limetangaza Alhamisi Juni 18 kwamba machafuko yanayoendelea kushuhudiwa nchini Burundi yamesababisha mpaka sasa vifo vya watu 70, kinyume na hamsini iliyotolewa iliyotolewa hivi karibuni.

Aprodh imebaini kwamba visa vya ukiukwaji wa haki za binadamu hususan mateso yanayowakabili waandamanji wanaozuiliwa katika jela mbalimbali za polisi na Idara ya upelelezi vimeendelea kushuhudiwa.

Hii ni ripoti ya kwanza ambayo inaonyesha idadi hiyo kubwa ya watu waliouawa katika maandamano dhidi ya muhula wa tatu wa rais Pierre Nkurunziza yaliyokumbwa na vurugu ziliyosababishwa, kwa mujibu wa Aprodh, na polisi kwa ushirikiano na maafisa wa Idara ya upelelezi.

Kiongozi wa shirika hilo, Pierre-Claver Mbonimpa, ameeleza idadi hiyo ya watu 70 waliyouawa ambayo ni kubwa kuliko ile inayojulikana mpaka sasa ya watu 50.

“ Mpaka sasa tunahesabu idadi ya watu 70 ambao wameuawa. Kuna watu wengine 500 ambao walijeruhiwa, na tuna idadi ya watu zaidi ya 500 wanaozuliwa katika jela tofauti. Kuna baadhi ya watu ambao wanazuliwa katika jela za polisi na Idara ya upelelezi ”, amesema Pierre-Claver Mbonimpa.

Miongoni mwa watu hao, kuna baadhi ya wanajeshi na askari polisi, hasa waandamanaji waliouawa kwa kupigwa risasi na vikosi vya usalama, lakini ni vigumu kusahihisha idadi hiyo ya watu 70, kwani polisi inakubali nusu ya idadi hiyo. Huenda polisi inatambua tu idadi ya watu wake waliouawa.

Pierre-Claver Mbonimpa hakuishia hapo, amebaini kwamba kati ya watu 800 na 1,000 wanazuiliwa katika jela mbalimbali. Amehakikisha kuwa wengi miongoni mwa wafungwa hao wanaendelea kufanyiwa mateso.

" Tunaona kwamba watu hao wanaokamatwa wanateswa. Aidha na polisi au Idara ya Upelelezi. Lakini nadhani, kama wanavyodai, ni kwa ajili ya kuwaadhibu ", ameongoza mwanaharakati huyo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.