Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 14/10 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 14/10 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 14/10 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Afrika

Misri: Morsi ahukumiwa adhabu ya kifo

media Rais wa zamani Morsi anaweza kukata rufaa dhidi ya hukumu mbili za Jumanne Juni16 mwaka 2015. REUTERS

Mahakama ya uhalifu ya Cairo imemuhukumu adhabu ya kifo rais wa zamani wa Misri Mohamed Morsi katika kesi inayojulikana kama " kutoroka jela ". Morsi alihukumiwa Jumanne wiki hii mapema saa moja kabla, kifungo cha maisha jela kwa kosa la "upelelezi". Mohamed Morsi anaweza kukata rufaa dhidi ya hukumu hizi.

Kwa mujibu wa mwandishi wa RFI, jijini Cairo, Alexandre Buccianti, Mahakama imempata rais wa zamani Mohamed Morsi na hatia ya kula njama katika uhalifu wa mauaji na kuendesha mashambulizi kwa kutumia silaha dhidi ya magereza nchini Misri Januari 29 mwaka 2011. Wakati huo, Morsi alikuwa kizuizini katika gereza la Wadi al-Natrun kaskazini mwa Cairo. Jela ambalo lilishambuliwa na watu wenye silaha, kwa mujibu wa Mahakama, watu hao walikuwa wafuasi wa Muslim Brotherhood, wafuasi wa Hamas kutoka Palestina, wafuasi wa Hezbollah kutoka Lebanon na wanajihadi kutoka Sinai.

Mapema leo Jumanne, mahakama hiyo ilimhukumu Bw Morsi, rais wa kwanza aliyechaguliwa kidemokrasia nchini Misri, kifungo cha maisha jela kwa kosa la " upelelezi " kwa maslahi ya Hamas kutoka Palestina, Hezbollah kutoka Lebanon na Iran. Machi 21, katika kesi ya kwanza, rais wa zamani wa Misri alikuwa alihukumiwa kifungo cha miaka ishirini jela kwa kosa la kuchochea vurugu dhidi ya waandamanaji mwaka 2012.

Rufaa

Kiogozi mkuu wa Muslim Brotherhood pia alihukumiwa adhabu ya kifo lakini kwa mara ya tatu. Watu hao waliohukumiwa wanaweza kukata rufaa dhidi ya hukumu ya Mahakama ya mwanzo katika kipindi cha siku sitini kwenye Mahakama ya ngazi ya juu. Kama rufaa yao inakubaliwa hukumu hiyo hufutwa na tarehe inapangwa kwa kesi mpya katika Mahakama ya uhalifu.

Zaidi ya wafuasi 600 wa Muslim Brotherhood walihukumiwa

Pamoja na hukumu zilizotolewa na mahakama Jumanne wiki hii, zaidi ya wafuasi 600 wa Muslim Brotherhood au washirika wao walihukumiwa adhabu ya kifo katika Mahakam ya mwanzo tangu kutimuliwa madarakani kwa rais wa zamani wa Misri, Mohamed Morsi mwezi Julai mwaka 2013. Mfuasi mmoja wa Muslim Brotherhood aliyepatikana na hatia ya mauaji ya kijana mmoja, aliuawa. Hukumu nyingi za kifo zilifutwa na Mahakama ya ngazi ya juu nchini Misri.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana