Pata taarifa kuu
CHAD-MASHAMBULIZI-USALAMA

Chad: mashambulizi ya kigaidi Ndjamena

Mji mkuu wa Cha, Ndjamena, umelengwa Jumatatu asubuhi wiki hii na mfululizo wa mashambulizi ya kujitoa mhanga. Milipuko kadhaa imesikika katika mji huo wa Chad.

Vikosi vya usalama vya Chad mbele ya kituo kikuu cha polisi cha Ndjamena kiliyolengwa na mashambulizi ya kigaidi Jumatatu Juni 15 mwaka 2015.
Vikosi vya usalama vya Chad mbele ya kituo kikuu cha polisi cha Ndjamena kiliyolengwa na mashambulizi ya kigaidi Jumatatu Juni 15 mwaka 2015. REUTERS/Moumine Ngarmbassa
Matangazo ya kibiashara

Milipuko ilitokea kwenye ofisi kuu ya Usalama wa umma, kwenye kituo kikuu cha polisi na karibu na shule ya polisi. Inasadikiwa kuwa watu 27 wameuawa na zaidi ya mia moja wamejeruhiwa.

Waziri wa mambo ya ndani wa Chad, amesema kuwa mashambulizi hayo yametekelezwa na watu wa kujitoa mhanga. Milipuko imesikika katika maeneo mengi ya mji wa Ndjamena ikilenga ofisi kuu ya Usalama wa umma na kituo kikuu cha polisi pamoja na shule ya polisi.

Mahahidi wa kwanza walio hojiwa na RFI, wamethibitisha hoja hiyo. Mmoja kati ya mashahidi, ambaye alikua karibu na kituo kikuu cha polisi, ameeleza kuwa shambulio limetokea muda mchache kabla ya saa nne. Shahidi huyo amebaini kwamba aliwaona watu wawili wakiwa kwenye pikipiki wakijielekeza kwenye kituo kikuu cha polisi, ambapo walizuiliwa na askari polisi. Wakati huo huo mmoja kati yao alijilipua na mwengine akatimka.

Mtu mwingine ambaye alikua amekuja kuangalia hati yake ya kusafiria, ametoa ushahidi wa mfululizo wa mashambulizi : " Hatukuelewa kilichotokea. Kulikuwa na mlipuko, kulikuwa na miili mingi ya watu waliopoteza maisha. Nilipatwa na mshituko wakati nilijikuta nikizungukwa na maiti. Polisi iliwasili haraka kwenye eneo la tukio, pamoja na magari mengi. Askari polisi walizuia barabara inayoelekea kwenye Ikulu".

Kwa upande wake waziri mkuu wa Chad, Kalzeubé Pahimi Deubet, amejielekeza leo Jumatatu mchana kwenye eneo kulikotokea mashambulizi mawili. Waziri huyo amethibitisha vifo vya watu 27 ikiwa ni pamoja na washambuliaji wanne, huku akibaini kwamba uchunguzi umeanzishwa na Ofisi ya mashtaka ya Mahakama ya Ndjamena ili kujaribu kujua ukweli kuhusu mashambulizi hayo.

Awali waziri wa habari wa Chad, Hassan Sylla, alibaini kwamba watu 27 ikiwa ni pamoja na washambuliaji wanne wameuawa na watu wengine 101 wamejeruhiwa.

Mpaka sasa hakuna kundi ambalo limekiri kutekeleza mashambulizi haya, licha ya kuwa kundi la Boko Haram linashukiwa kufanya hivyo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.