Pata taarifa kuu
MADAGASCAR - SIASA

Mahakama yatupilia mbali ombi la bunge la kutokuwa na imani na rais

Mahakama nchini Madagascar imetupilia mbali ombi la bunge la kutokuwa na imani na rais wa nchi Hery Rajaonarimampianina baada ya kupiga kuwa na bunge la nchi hiyo. Mahakama ya kikatiba imesema tuhuma dhidi ya rais hazina msingi wa kisheria na hivyo wametupilia mbali ombi hilo la kuondolewa kwa rais.

Mahakama kuu ya kikatiba.
Mahakama kuu ya kikatiba. AFP PHOTO / RIJASOLO
Matangazo ya kibiashara

Pierre Houlder msemaji wa chama cha rais wa zamani wa nchi hiyo Andry Rasjoelina amesema uamuzi wa mahakama unatia aibu, kwa sababu idadi kubwa ya wabunge walipiga kura Mei 28 mwaka huu walionyesha kutokuwa na imani na rais hivyo alitakiwa kuondolewa madarakani.

Upande wake mwenyekiti w chama cha rais Hery Rivo Rakotovao, amesema wapo katika utawala wa sheria, hivyo wanasiasa wote wanatakiwa kuheshimu uamuzi wa mahakama hiyo.

Wakati huo huo naibu mwenyekiti wa chama cha MPAR cha rais wa zamani wa nchi hiyo aNDRY rajoelina, Augustin Andriamananoro amesema sluhusu ya mzozo wa Madagascar sasa utatatuliwa na wananchi kwa kuandaa uchaguzi kabla ya wakati.

Rais huyo anakbiliana na upinzani kutoka pande mbili za ma rais wa zamani wa nchi hiyo ambao walitengwa katika mchakato wa uchaguzi wa mwaka 2013 kutokana na shinikizo la kimataifa

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.