Pata taarifa kuu
G7-MAZINGIRA-UCHUMI-UGAIDI

Viongozi wa G7 wakubaliana kuzuia kusambaa kwa gesi chafu

Mkutano wa mataifa saba yenye uwezo mkubwa wa kiuchumi Duniani (G7), Marekani, Ujerumani, Japan, Ufaransa, Uingereza, Italia na Canada, umemalizika Jumatatu Juni 8 katika Elmau Castle, hoteli ya kifahari katika milima ya Bavaria.

Viongozi wa nchi za G7 na wageni wao wamekusanyika katika Elmau Castle katika milima ya Bavaria, tarehe 7 na 8 Juni mwaka 2015.
Viongozi wa nchi za G7 na wageni wao wamekusanyika katika Elmau Castle katika milima ya Bavaria, tarehe 7 na 8 Juni mwaka 2015. REUTERS/Christian Hartmann
Matangazo ya kibiashara

Baada ya Ukraine, ambayo ilishiriki mazungumzo ya Jumapili, mkutano wa hali ya hewa (COP 21) utakaofanyika mjini Paris mwishoni mwa mwaka 2015 na deni la Ugiriki ni miongoni mwa masuala amabyo yaliulizwa katika mijadala.
Mazingira

Nchi wanachama wa G7 zimekubaliana Jumatatu wiki hii kupunguza kiwango cha carbon katika uchumi wao, ili kuidhinisha lengo la kupunguza uzalishaji wa gesi chafu duniani. Hata hivyo, hakuna nchi hata moja imejikubalisha hatua za kisheria. Jambo ambalo litazifurahisha nchi za Japan na Canada, nchi hizi mbili zinazokataa kukaguliwa. Lakini mashirika yasiyo yakiserekali yaliyoshiriki mkutano huu yameonekana kukaribisha matokeo ya mkutano huu.

" G7 imeonesha ishara kwamba zama za nishati zimekua juu ", afisa wa masuala ya hewa katika shirika la Greenpeace amesema.

“ Leo, hatua za kisheria hazipo. Hii itakuwa ni lengo la mkutano wa Paris ”, Kansela wa Ujerumani Angela Merkel, amesema.

Lengo lililo wazi, ni lile la kupunguza ongezeko la wastani wa joto duniani hadi mwaka 2100 kufikia kiwango cha 2 ° C ikilinganishwa zama kabla ya viwanda. Kutokana na hali hiyo, nchi hizo zinalenga asilimia 40-70 ya uzalishaji wa gesi chafu chini ya kiwango cha kimataifa ifikapo mwaka 2050. Uamuzi ambao umekaribishwa na François Hollande, ambaye amesifu "makubaliano kababmbe na yenye uhakika" katika mapambano dhidi ya ongezeko la joto duniani, katika mkutano utakaofanyika mwezi Desemba jijini Pris, nchini Ufaransa.

    • Ukraine

Viongozi wa mataifa saba yenye uwezo mkubwa wa kiuchumi Duniani-G7, wamekubaliana kuwa vikwazo dhidi ya Urusi vinafaa kuendelea.
Bi Merkel amesema hadi pale muafaka wa kukomesha mapigano nchini Ukraine utakapoheshimiwa vikwazo sharti ziendelee.
Akiongea katika siku ya mwisho ya mkutano wa siku mbili, Merkel amesema kuwa mataifa ya G7 yalikuwa tayari kuzidishia Urusi vikwazo zaidi, iwapo hali ingeruhusu.

   • Ugaidi

Viongozi kutoka Nigeria na Tunisia wamedhuria mkutano huu, na suala linalohusiana na hatari inayosababishwa na makundi yenye itikadi kali hasa yale ya Afrika limezungumziwa. Viongozi wa G7 wamesema kuunga mkono muungano wa kimataifa unaoongozwa na Marekani dhidi ya Islamic State nchini Iraq na Syria, huku wakiwa na matumaini ya kulishinda kundi hili.

   • Ugiriki

Kuhusu mzozo wa kifedha unaokumba Ugiriki, Barack Obama aligusia sualala deni la Ugiriki. Naye Bi Merkel, alionya kuwa muda uliosalia kabla makubaliano hayajatiwa sahihi ni mchache mno. Alishauri Ugiriki kuchukua hatua madhubuti ilikunusuru sarafu ya taifa hilo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.