Pata taarifa kuu
BURUNDI-SIASA-USALAMA

Shughuli za Ceni zakwama, kufuatia kujiuzulu kwa wajumbe wake 2

Hali ya kisiasa na usalama nchini Burundi imeendelea kuwa tete. Uchaguzi wa Wabunge na Madiwani umekua unatazamiwa kufanyika rasmi Ijumaa Juni 5, lakini sasa haijulikani iwapo utafanyika au la.

Tume huru ya Uchaguzi Burundi (Ceni), inakabiliwa na changamoto ya kuandaa uchaguzi  kufuatia kujiuzulu kwa wajumbe wake wawili, zikisalia siku tatu za uchaguzi wa Wabunge na Madiwani. Hapa, Rais Nkurunziza wakati kuwasilisha faili yake kwenye Ceni.
Tume huru ya Uchaguzi Burundi (Ceni), inakabiliwa na changamoto ya kuandaa uchaguzi kufuatia kujiuzulu kwa wajumbe wake wawili, zikisalia siku tatu za uchaguzi wa Wabunge na Madiwani. Hapa, Rais Nkurunziza wakati kuwasilisha faili yake kwenye Ceni. RFI/SR
Matangazo ya kibiashara

Jumapili Mei 31, viongozi wa nchi za jumuiya ya Afrika Mashariki walikutana na kuchukua uamzi wa kuitaka serikali ya Burundi na Tume huru ya Uchaguzi (Ceni) kuahirisha kwa kipindi cha mwezi mmoja na nusu uchaguzi huo.

Tume Huru ya Uchaguzi, kwa upande wake, imeendelea kuhakikisha kuwa inaendesha kazi yake kama kawaida licha ya kujiuzulu kwa naibu mwenyekiti wa Tume hiyo, Spes-Caritas Nirondoye, pamoja na mkurugenzi wa masuala ya utawala na fedha, Illuminata Ndabahagamiye. Lakini kujiuzulu kwa watu hao ni tatizo kubwa kwa utendaji kazi wa Tume hiyo ya Uchaguzi.

Hakuna matatizo yoyote kuhusu kuahirishwa kwa uchaguzi. Rais Nkurunziza anatazamiwa kusaini sheria baada ya kukutana na kushauriana na Tume huru ya Uchaguzi (Ceni). Iwapo kuahirishwa kutathibitishwa, kuahirishwa kwa uchaguzi kutatangazwa na Tume huru ya Uchaguzi.

Hata hivyo tume huru ya Uchaguzi bado inakabiliwa na matatizo ya utendaji kazi, baada ya kujiuzulu kwa wajumbe wake wawili kwa jumla ya wajumbe watano wanaounda Tume hiyo.

Hata hivyo, Tume huru ya Uchaguzi inapaswa kuchukua maamuzi ya kuandaa uchaguzi kwa makubaliano ya wajumbe wote au kwa idadi kubwa ya wajumbe 4 kwa jumla ya watano wanaounda Ceni.

Kutokana na hali hiyo italazimika kuwateua watu wengine wawili watakaochukua nafasi ya wajumbe hao wawili waliojiuzulu. Na kwa mujibu wa Katiba, inahitaji sheria ya rais baada ya watu hao kupasishwa kwa asilimia 75 ya Wabunge na Maseneta.

Wabunge na maseneta wameanza kukutana katika vikao mbalimbali tena kuanzia Jumatatu, Juni 1, zikisalia siku 3 za uchaguzi wa wabunge na Madiwani kufanyika kulingana na kalenda ya uchaguzi ya zamani. Hali hii imewashangaza wengi wakati Baraza la Bunge na Seneti vilimaliza muhula wao tangu Aprili 30.

Kinachosalia ni kujua iwapo serikali itafanikiwa kukusanya asilimia 75 za kura kwa kuweza kuwapitisha wagombea hao kwenye nafasi za wajumbe wa Ceni waliojiuzulu, hasa kwa upande wa Baraza la Bunge.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.