Pata taarifa kuu
FIFA-SOKA-SHERIA

Sepp Blatter achaguliwa kwa mara nyingine kuingoza Fifa

Sepp Blatter amechaguliwa kwa mara nyingine tena Ijumaa wiki hii kuliongoza Shirika la Soka Duniani (Fifa) katika mkutano wa 65 wa Shirikisho hilo la kandanda Duniani.

Sepp Blatter achaguliwa kwa mara nyingine tena kwa muhula wa tano kwenye uongozi wa Fifa.
Sepp Blatter achaguliwa kwa mara nyingine tena kwa muhula wa tano kwenye uongozi wa Fifa. REUTERS/Arnd Wiegmann
Matangazo ya kibiashara

Sepp Blatter amechaguliwa katika duru ya pili baada ya mshindani wake mwanamfalme Ali Bin Al Hussein kujiondoa katika kinyanga'nyiro hicho.

Sepp Blatter mwenye umri wa miaka 79, analiongoza Shirikisho la Soka Duniani kwa muhula wa tanu sasa, tangu mwaka 1998.

Katika duru ya kwanza ya uchaguzi huo, mshindi hakupatikana baada ya kukosekana kwa alama zilizokua zinahitajika. Awali Sepp Blatter alipata kura 133 huku mshindani wake ambaye ni mwanamfalme Ali Bin Al Hussein akipata kura 73. Kura 140 ndizo zilikua zinahitajika ili aweze kupatiukana mshindi.

“ Ninaahidi kumkabidhi mrithi wangu Fiafa yenye nguvu ”, amesema Sepp Blatter baada ya kuchaguliwa kwake kuwa rais wa Shirikisho la Soka Duniani, ambalo linakabiliwa na kimbunga kikali baada ya maafisa wake kadhaa wa zamani kutuhumiwa kashfa ya rushwa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.