Pata taarifa kuu
Watu saba wauawa wilayani Beni mashariki mwa DRC

Waasi wa ADF waua watu saba mjini Beni mashariki wma Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo

Takribani maiti saba zimepatikana katika mji wa Matembo karibu na mji wa Beni mashariki mwa jamuhuri ya demokrasia ambako kumeshuhudia mfulululizo wa mauaji ambayo watu mia 3 waliuawa katika kipindi cha miezi 7,mamlaka zimebainisha.

Familia za watu wakiomboleza jamaa waliouawa mjini Beni, tarehe 9 mei 2015.
Familia za watu wakiomboleza jamaa waliouawa mjini Beni, tarehe 9 mei 2015. AFP PHOTO / KUDRA MALIR
Matangazo ya kibiashara

Mpiga picha wa shirika la habari AFP ameshuhudia miili saba ambapo miwili ni wanawake wakati ilipofikishwa katika chumba cha kuhifadhia maiti mjini Beni.

Gavana wa jimbo la kivu ya kaskazini Julien Paluku, amethibitisha kupatikana kwa miili hiyo katika mji wa matembo eneo la Mulekera kilomita chache kutoka mjini Beni, kuelekea kwenye uwanja wa ndege wa Mavivi.Hata hivyo gavana huyo kasema bado haijajulikana ikiwa mauaji hayo yalifanywa na waasi wa Uganda ADF.

Mashuhuda wanasema maiti hizo zikiwa na majeraha ya kushambuliwa kwa mapanga, shoka na majambia.

Katika akaunti yake ya twitter gavana huyo amesema mauaji hayo yamechosha na kwamba amekuwa akisikitikia ukimya wa serikali ya Kinshasa na umoja wa mataifa unaowakilishwa nchini humo kushindwa kuzuia mauaji hayo, haswa kwa watu wa jamii ya wanande.

Kaongeza kuwa ni jambo lisiloeleweka kuona heshima zinazotolewa kwa askari wawili wa umoja wa mataifa waliouawa huko Beni hivi majuzi hazipewi kwa makumi ya watu wanaoendelea kuuawa katika eneo hilo.

Waasi wa kiislamu wa ADF ambao walianzisha uasi katika nchi jirani ya Uganda dhidi ya raisi Museven wanatuhumiwa kutekeleza mfululizo wa mashambulizi jirani na mji wa Beni na kusababisha vifo vya takribani watu mia 3 tangu mwezi Octoba mwaka jana.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.