Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 18/07 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 18/07 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 17/07 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Afrika

Suala la ugaidi lawagawanya wabunge Kenya

media Wanajeshi wa Kenya wakiwasili katika Chuo kikuu cha garissa, kulikotokea shambulio la kigaidi lililogharimu maisha ya watu 148, ikiwa ni pamoja na wanafunzi 142. à l'université de Garissa, le 4 avril. REUTERS/Goran Tomasevic

Nchini Kenya, baadhi ya wabunge wanamshinikiza kiongozi wao bungeni Aden Duale kujiuzulu baada ya kusema kuwa kwa muda wa mwezi mmoja ujao atatoa orodha ya watu wanaoshirikiana na kundi la kigaidi la Al Shabab kutoka Somalia.

Wabunge hao wamesema, viongozi kutoka Kaskazini Mashariki mwa Kenya wanachukua muda mrefu kutoa majina hayo na kusisitiza kuwa Duale ajiuzulu wadhifa wake kabla ya kutoa majina hayo.

Hata hivyo, Duale amesema hatajiuzulu na kueleza kuwa wanasiasa kutoka Kaskazini mwa nchi hiyo wanafanya bidii kuhakikisha kuwa wanapigana na ugaidi.

Wakati huo huo mjadala unaendelea nchini Kenya ikiwa vijana waliojiunga na kundi la Al Shabab nchini Somalia waliopewa siku 10 wajisalimishe na kusamehewa ikiwa itakuwa ni sahihi kusamehewa.

Baadhi ya wabunge nchini humo wmeasema ikiwa watajisalimisha wachukuliwe hatua huku viongozi wa Kiislamu wakitaka serikali kuongeza muda huo.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana