Pata taarifa kuu
KENYA-SHABAB-MASHAMBULIZI-USALAMA

Ndege za Kenya zashambulia kambi mbili za Al Shabab

Ndege za kijeshi za Kenya zimeendesha mashambulizi Jumatatu wiki hii dhidi ya kambi mbili za wanamgambo wa kiislamu wa Al Shabab, nchini Somalia, msemaji wa jeshi la Kenya ameliambia shirika la habari la Ufaransa AFP.

Jeshi la Kenya limeendesha mashambulizi dhidi ya kambi mbili za wanamgambo wa kiislamu wa Al Shabab, Somalia, Aprili 6 mwaka 2015.
Jeshi la Kenya limeendesha mashambulizi dhidi ya kambi mbili za wanamgambo wa kiislamu wa Al Shabab, Somalia, Aprili 6 mwaka 2015. REUTERS/Gregory Olando
Matangazo ya kibiashara

Kundi la Al Shabab lilikiri hivi karibuni kuhusika katika mashambulizi dhidi ya Chuo kikuu cha Garissa, nchini Kenya. Mashambulizi ambayo yaligharimu maisha ya watu 148.

“ Tumeshambulia kambi mbili za wanamgambo wa kiislamu wa Al Shabab katika mkoa wa Gedo, karibu na mpaka na Kenya”, amesema msemaji wa jeshi la Kenya, David Obonyo.

“ Kambi hizo mbili zimeshambuliwa, na kuteketezwa moja kwa moja”, ameongeza Obonyo, bila hata hivyo kutoa maelezo zaidi.

Obonyo ameeleza kwamba mashambulizi dhidi ya kambi hizo mbili yalikua yalipangwa hata kabla ya mashambulizi dhidi ya Chuo kikuu cha Garissa. Obonya ameahidi kwamba mashambulizi hayo yataendelea, mpaka pale kundi hili litaamua kujisalimisha au kuangamia.

Jeshi la Kenya liliingia nchini Somalia mwezi Oktoba mwaka 2011 kwa lengo la kupambana dhidi ya wanamgambo wa Al Shebab. Wakati huo wanajeshi wa Kenya waliingizwa katika kikosi cha wanajeshi wa Umoja wa Afrika wanaosimamia amani nchini Somalia (Amisom) tangu mwaka 2007 kwa lengo la kutoa msaada kwa vikosi dhaifu vya Somalia na kuendesha vita dhidi ya kundi la Al Shebab, ambalo kwa sasa linakadiriwa kuwa na wapiganaji 22,000.

Tangu mwishoni mwa mwaka 2011 kundi hili la Al Shabab lilizidisha mashambulizi katika ardhi ya Kenya kwa kulipiza kisasi kuingia kwa majeshi ya Kenya Somalia. Mashambulizi ambayo yamewauwa watu wengi nchini Kenya.

Mashambulizi ya Chuo kikuu cha Garissa ni mashambulizi ya kwanza ambayo yamesababisha maafa makubwa tangu mashambulizi dhidi ya ubalozi wa marekani mjini Nairobi, mashambulizi ambayo yaliendeshwa na mtandao wa Al-Qaeda, ambapo Al Shebab ni moja ya makundi yanayo uhusiano na kundi hili la Al Qaeda. Mashambulizi hayo dhidi ya ubalozi wa Marekani mjini Nairobi yalisababisha vifo vya watu 213 mwaka 1998.

Kabla ya shambulio dhidi ya Chuo kikuu cha Garissa, Al Shabab ilikiri kuhusika katika mashambulizi dhidi ya kitua cha biashara cha Westgate mwezi Septemba mwaka 2013, mashambulizi ambayo yaligharimu maisha ya watu 67.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.