Pata taarifa kuu
BURUNDI-SIASA

Mpasuko waendelea kushuhudiwa katika chama cha CNDD-FDD kuhusu muhula wa 3

Mgawanyiko umeendelea kushuhudiwa katika chama tawala cha Cndd-Fdd nchini Burundi kuhusu muhula wa 3 wa rais Pierre Nkurunziza. 

Leonidas Hatungimana, msemaji wa rais Nkurunziza
Leonidas Hatungimana, msemaji wa rais Nkurunziza
Matangazo ya kibiashara

Mgawanyiko huu unajitokeza kutokana na baadhi ya wanachama na viongozi wa chama hicho kinacho tawala kumuandikia barua rais Pierre Nkurunziza wakimtaka kutowania muhula wa tatu wa urais kwenye uchaguzi unaokuja wakati huu kukiwa na wasiwasi kuwa huenda kiongozi huyo akagombea tena.

Baadhi ya viongozi katika taasisi mbalimbali za serikali ya Burundi, wakiwa pia wafuasi wenye ushawishi mkubwa katika chama madarakani nchini humo cha CNDD-FDD akiwemo Leonidas Hatungimana ambae ni msemaji wa rais Pierre Nkurunziza, Onesime Nduwimana msemaji wa Chama tawala, Geevieve Kanyage mkuu wa tawi la akina mama katika chama cha cndd-fdd, pamoja na wengine 9 wanaoshikilia nyadhifa mbalimbali.

Viongozi hao wamebaini katika barua hiyo kwamba kulingana na hali inayojiri kwa sasa nchini Burundi kufuatia hatuwa ya rais Nkurunziza kutaka kuwania muhula wa 3, viongozi hao wameamuwa kuvunja ukimya na kujiunga na wazee wa busara katika chama na kumtaka rais Nkurunziza kubadili msimamo wake wa kutaka kuwania muhula mwingine wa 3, ili kukuweka pazuri chama hicho na kuangalia vizuri na jumuiya ya kimataifa.

Willy Nyamitwe afisaa wa habari katika jopo la maandalizi ya uchaguzi katika chama cha Cndd-Fdd amepuuzia barua hiyo na kubaini kwamba ni barua ya kawaida na haiwatetereshi, haiwezi kusababisha mpasuko, kwani hata watu wengine wanaweza kujitokeza na kuandika barua kama hiyo.

Hata hivyo wananchi wa Burundi wanaonakuwa ni wakati muafaka sasa kwa rais Nkurunziza kubaini msimamo wake wakati huu akiendelea kushauriwa na watu kutoka ndani na nje ya Burundi kutowania muhula mwingine wa tatu kutokana na jambo hili kuwa kinyume na katiba ya Burundi.

Kulingana na wataalamu wa ndani na nje ya Burundi wanaonakuwa hatuwa ya rais Nkurunziza kuwania muhula wa 3 inaweza kuzuia machafuko katika nchi hiyo iliowahi kushuhudiwa machafuko ya kikabila miaka kadhaa ya nyuma.

Viongozi mbalimbali kutoka chama hicho wamekuwa wakiondolewa kwenye nyadhifa zao na wengine kufukuzwa chamani kutokana tu na kubaini msimamo wao wa kupinga muhula wa 3 wa rais Nkurunziza.

Hayo yakijiri, msemaji wa chama cha Cndd-Fdd, Onesime Nduwimana, amefutwa kwenye nafasi hiyo. Uamzi unakuja baada ya msemaji huyo wa chama madarakani kutoa msimamo wake kwamba rais Pierre Nkurunziza sio mgombea pekee katika chama hicho.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.