Pata taarifa kuu
TUNISIA-UGAIDI-USALAMA

Maandamano makubwa Tunis: “Muungano wa kitaifa” dhidi ya ugaidi

Maandamano mapya yanayojumuisha mamia ya watu yanatazamiwa kufanyika Ijumaa wiki hii katika mji mkuu wa Tunisia, Tunis, mbele ya makavazi ya Bardo jijini Tunis, ambapo shambulio la kigaidi liligharimu maisha ya watu 21.

Mwanamke wa Tunisia akibeba bango lililoandikwa kwa herufi za ishara ya damu mjini Tunis: " hapana kwa ugaidi" , Machi 19 mwaka 2015.
Mwanamke wa Tunisia akibeba bango lililoandikwa kwa herufi za ishara ya damu mjini Tunis: " hapana kwa ugaidi" , Machi 19 mwaka 2015. AFP PHOTO / FADEL SENNA
Matangazo ya kibiashara

Raia wa kigeni 20 pamoja na raia mmoja wa Tunisia ni miongoni mwa waliouawa. Watu zadi ya arobaini walijeruhiwa katika shambulio hilo.

Awali maandamano kama hayo yaliandaliwa na asasi thelathini pamoja na chama kikuu cha wafanyakazi nchini Tunisia (UGTT), huku kauli mbio ikiwa “ Umoja wa kitaifa”dhidi ya ugaidi.

Rais wa Tunisia Beji Caïd Essebsi, kwa upande wake ametangaza kwamba wauaji walioendesha shambulio hilo katika makavazi ya Bardo walikua walivalia “ vilipuzi” na vikosi vya usalama viliwahi kuzima shambulio hilo kwa “ kuepuka janga kubwa” ambalo lingeweza kutokea kutokana na vilipuzi hivyo.

Baadhi ya waandamanaji waliweka shada za maua na mishumaa kwenye eneo la tukio kwa kutoa rambirambi zao kwa wahanga.

Mokthar Trifi, kiondozi wa zamani wa shirika la haki za binadamu nchini Tunisia, ambaye alikua alishiriki maandamano hayo alisema raia wote wa Tunisia wameungana na kusema “ hapana” kwa ugaidi.

Kundi la wapiganaji wa Dola la Kiislamu limekiri kutekeleza shambulio hilo dhidi ya makavazi ya Bardo mjini Tunis, lililogharimu maisha ya watu 21, wengi wao wakiwa watalii.

Washukiwa tisa walikamatwa Alhamisi wiki hii, kwa mujibu wa Ikulu ya Tunis. Watu hao wanasadikiwa kuwa walikua wakiwasiliana na wauaji hao walioendesha shambulio katika makavazi ya Bardo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.