Pata taarifa kuu
SIERRA LEONE-SIASA

Ernest Bai Koroma amteua makamo mpya wa rais

Rais wa Sierra Leone Ernest Bai Koroma amemteau Makamu mpya wa rais baada ya kumfuta kazi Samuel Sam-Sumana.

Ernest Bai Koroma, rais wa Sierra-Leone.
Ernest Bai Koroma, rais wa Sierra-Leone. (Photo : AFP)
Matangazo ya kibiashara

Rais Koroma amemteua Victor Bockarie Foh, ambaye alikuwa Balozi wa Sierra Leone nchini China kushikilia wadhifa huo haraka iwezekanavyo.

Mbali na kuwa Balozi, Foh aliwahi wakati mmoja kuwa katibu mkuu wa chama tawala cha APC kwa muda wa miaka kumi, kabla ya kwenda nchini China kuiwakilisha nchi yake.

Wakati huo huo Samuel Sam-Sumana naye amesema atakwenda katika Mahakama ya juu kupinga uamuzi wa kufutwa kazi na rais Koroma.
Sumana amesema, rais Koroma amekiuka kwa kumfuta kazi kwa sababu hakumteua, lakini alichaguliwa pamoja naye kama mgombea mwenza.

Taarifa kutoka Ikulu jijini Freetown zimesema kuwa Sumana alifutwa kazi baada ya kuomba hifadhi ya kisiasa katika ubalozi wa Marekani juma moja lililopita kwa madai ya kuhofia maisha yake baada ya kufukuzwa katika chama tawala cha APC.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.