Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 18/01 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 17/01 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 17/01 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Afrika

Watu watatu wauawa katika shambulio dhidi ya Minusma Kidal

media Wanajeshi wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa wakipiga doria katika mji wa Kidal, mwezi Julai mwaka 2013. AFP PHOTO / KENZO TRIBOUILLARD

“ Kambi ya vikosi vya kulinda amani vya Umoja wa Mataifa nchini Mali (Minusma), imeshambuliwa Jumapili Machi 8 kwa makombora zaidi ya thelathini”, kikosi cha Umoja wa mataifa nchini Mali kimetangaza katika tangazo kiliyotoa Jumapil hii.

Hata hivyo kikosi cha Umoja wa Mataifa nchini Mali kimebaini kwamba kimeweza kujibu shambulio hilo. Shambulio ambalo limegharimu maisha ya watu watatu ikiwa ni pamoja na mwanajeshi mmoja wa kikosi cha Umoja wa Mataifa na raia wawili wa kawaida, huku zaidi ya watu 20 ikiwa ni pamoja na wanajeshi wanane wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa wakijeruhiwa.

Shambulio hilo linatokea siku moja kabla ya kutokea kwa machafuko katika mji wa Gao.

Shambulio la kwanza lilitokea mapema asubuhi kabla ya kuzimwa na wanajeshi wa kikosi cha Umoja wa Mataifa. Lakini muda mchache baadae, shambulio jingine limetokea katika eneo kunakopatikana kambi ya kikosi cha wanajeshi wa Umoja wa Mataifa.

Wanajeshi wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa, ambao ni washirika wa kikosi cha wanajeshi wa Ufaransa Barkhane katika eneo hilo wamejibu shambulio na kufanikiwa kulizima.

Katika hali ya kubadilishana risasi, baadhi ya makombora yaliangukia katika eneo linalokaliwa na raia, karibu kilomita tatu na kambi hiyo ya kikosi cha wanajeshi wa Umoja wa Mataifa katika mji wa Kidal, na kupelekea watoto wawili kufariki. Upande wa Minusma mwanajeshi mmoja kutoka Chad ameuawa.

Hali hii imezua mvutano mkubwa baina ya viongozi na raia, ambapo maswali yamekosa majibu. Baadhi wanajiuliza iwapo makombora hayo yaliyorushwa hadi katika eneo linalikaliwa na raia yametokea katika kambi ya kikosi cha wanajeshi wa Umoja wa Mataifa, huku wengine wakijiuliza iwapo makombora hayo yalitokea upande wa kambi ya wanamgambo wa kiislamu.

Kundi la wanajihadi linaloendesha harakati zake nchini Algeria Mali Mokhtar Belmokhtar, linadaiwa kuwa ndilo limetekeleza mashambulizi hayo dhidi ya kambi ya wanajeshi wa kikosi cha Umoja wa Mataifa nchini Mali.

Umoja wa Mataifa umelani mashambulizi hayo dhidi ya kambi ya wanajeshi wake. Mashambulizi ambayo yamegharimu maisaha ya watu watatu, ikiwa ni pamoja na mwanajeshi mmoja wa kikosi hicho kutoka Chad pamoja na watoto wawili.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana