Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 16/02 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 16/02 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 16/02 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Afrika

FARDC yashambulia waasi wa FDLR

media Mwanajeshi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, akiangalia jinsi gari la aliyekua mkuu wa jeshi la DRC mashariki mwa Congo, Mamadou N'dala Moustapha lilkiteketea kwa moto. REUTERS/Kenny Katombe

Jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo limetangaza kwamba limeanzisha operesheni kabambe dhidi ya waasi wa Kihutu wa Rwanda wa FDLR

wanaoendesha harakati zao mashariki mwa nchi hiyo.

Waasi hao wa FDLR wanatuhumiwa kutekeleza uhalifu mkubwa dhidi ya binadamu. Jeshi la Jamhuri ya Kidemmokrasia ya Congo (FARDC) linaendesha operesheni hiyo dhidi ya waasi wa FDLR bila msaada wowote wa Umoja wa Mataifa.

Msemaji wa jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, jenerali Léon Richard Kasonga, amehakikisha kuwa jeshi limedhibiti hali ya mambo.

Hivi karibuni Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia Congo, Joseph Kabila, alisema akisisitiza mbele ya mabalozi 21 wa jumuiya ya kimataifa nchini humo, ikiwa ni pamoja na mkuu wa ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini DRC, kwamba nchi yake haihitaji tena msaada wa Umoja wa Mataifa ili kupambana na waasi wa FDLR.

Katika mkutano ambao haukuashiria hali ya mazungumzo ya kawaida, Rais Kabila alikosoa tabia ya mabalozi hao kuingilia masuala ya ndani ya nchi yake, huku akitangaza kutohitaji tena msaada wowote wa kijeshi kutoka kwa askari wa kulinda amani wa Umoja wa mataifa nchini humo MONUSCO.

Wiki moja kabla ya mkutano huo kati ya Rais Kabila na mabalozi kutoka jumuiya ya kimataifa, Ujumbe wa umoja wa mataifa MONUSCO ulitangaza kusitisha msaada wowowte wa kijeshi kupambana na waasi hao ili kupinga uteuzi wa majenerali wawili wanaotuhumiwa kutekeleza vitendo vya uhalifu nchini humo, tuhuma ambazo zinaendelea kutipiliwa mbali na serikali ya Congo.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana