Pata taarifa kuu

Mkutano mpya wa kuboresha mkakati dhidi ya Boko Haram

Viongozi wa nchi za Afrika ya Kati wanakutana katika mkutano wa dharura Jumatatu wikii katika mji mkuu wa cameroon, Yaounde kuboresha mkakati wa pamoja dhidi ya Boko Haram.

Paul Biya, Rais wa Cameroon, mwenyeji wa mkutano huo, na viongozi wenzake watajadili kwa kina majukumu ya kikosi cha kikanda cha kupambana dhidi ya Boko Haram.
Paul Biya, Rais wa Cameroon, mwenyeji wa mkutano huo, na viongozi wenzake watajadili kwa kina majukumu ya kikosi cha kikanda cha kupambana dhidi ya Boko Haram. AFP PHOTO / REINNIER KAZE
Matangazo ya kibiashara

Kwa jumla, nchi kumi wanachama wa Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Afrika ya Kati wanataka kuonyesha umoja wao juu ya suala hilo. miongoni mwa mada zitakazojadiliwa katika mkutano huo ni pamoja na kuunda jeshi la pamoja la kanda hiyo.

Mkutano huu ni sehemu ya mchakato wa muda mrefu ambao una lengo la kuunda vikosi vya majeshi ya Afrka na hasa kuweka wazi utaratibu na muhula kikosi hicho cha kikanda, ambacho kimo mbioni kuundwa.

Wataalamu wa kijeshi walikutana katika mji wa Yaounde kufafanua sheria za kushiriki katika kikosi hiki cha kikanda ambacho kitaundwa na wanajeshi 8,700 (kutoka Chad, Cameroon, Nigeria na Benin).

Lakini mpango utawasilishwa kwa Baraza la Amani na Usalama la Umoja wa Afrika na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.

Mbali na masuala ya kisheria, Cameroon na Chad, nchi mbili ambazo ziko kwenye mstari mbele katika vita dhidi ya kundi la Boko Haram ziko tayari kuhakikisha kuwa kundi hilo ziimelitokomeza.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.