Pata taarifa kuu
KENYA-SHAMBULIO-USALAMA

Shambulio moja lawajeruhi watu watatu Mandera

Watu watatu wamejeruhiwa baada ya kutokea kwa mlipuko wa guruneti katika mgahawa mmoja mjini Mandera, kaskazini mashariki mwa Kenya

Kaunti ya Mandera, nchini Kenya, yaendelea kushuhudia mashambulizi. Watu watatu wajerihiwa katika shambulio lilitokea katika Kaunti hiyo, Alhamisi jioni, Februari 5 mwaka 2015.
Kaunti ya Mandera, nchini Kenya, yaendelea kushuhudia mashambulizi. Watu watatu wajerihiwa katika shambulio lilitokea katika Kaunti hiyo, Alhamisi jioni, Februari 5 mwaka 2015. REUTERS/Stringer
Matangazo ya kibiashara

Mlipuko huo ulitokea Alhamisi jioni wiki hii, kwa mujibu wa taarifa za polisi, na majeruhi hao wanaendelea kupata matibabu katika hospitali ya mji wa Mandera.

Job Boronjo, Kamanda wa polisi katika Kaunti ya Mandera ameliambia Gazeti la kila siku nchini humo kwamba polisi wanatafuta watu waliohusika na urushaji wa guruneti hiyo.

Mkuu huyo wa polisi katika Kaunti ya Mandera ameongeza kuwa maafisa wake wako makini kutokana na vitisho vya kundi la Al Shabab kutoka nchini Somalia kuendelea kutishia kutekeleza mashambulizi katika eneo hilo.

Haya ndio mashambulizi ya haivi karibuni kuripotiwa katika eneo hilo karibu na Somalia, na yanakuja wakati huu walimu wanaofanya kazi katika Kaunti hiyo wakiendelea kususia kurudi kazini kwa hofu ya usalama.

Mwaka jana, mashambulzi mawili yaliyokea katika Kaunti hiyo ya Mandera baada ya abiria 28 kuuawa katika mashambulizi yaliyoendeshwa na Al Shabab wakiwa njiani kwenda jijini Nairobi na wachimba migodi 36 kuuawa baada ya kuvamiwa na kushambuliwa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.