Pata taarifa kuu
CAR-ANTI BALAKA-SELEKA-Usalama

Wafuasi wa makundi hasimu wafikia makubaliano

Makubaliano yanayolenga kusitisha machafuko nchini Jamhuri ya Afrika ya kati yametiwa saini kati ya wafuasi wa marais wa zamani Michel Djotodia na François Bozizé jijnii Nairobi nchini kenya.

Wanamgambo wa kundi la  kikristo la Anti-balaka wakipora duka la mfanyabiashara kutoka jamii ya Waislamu, mjini Bangui.
Wanamgambo wa kundi la kikristo la Anti-balaka wakipora duka la mfanyabiashara kutoka jamii ya Waislamu, mjini Bangui. © Pierre Terdjman Exposition produite par Paris Match
Matangazo ya kibiashara

Viongozi hao waliokutana mjini humo tangu mwishoni mwa mwezi Desemba wamehitimisha majadiliano hayo siku ya Jumanne kwa niaba ya kundi la waasi wa zamani wa Seleka ambao sasa wanajiita FPRC na ujumbe wa wanamgambo wa Anti- Balaka.

Makubaliano hayo yenye kurasa kumi na tano yanadaiwa kutetea mchakato wa amani nchini jamhuri ya Afrika ya Kati kwa njia ya mpango wa DDR unaolenga kuwapokonya silaha wapiganaji hao na kuwaunganisha na jamii, pamoja na kuunda jeshi litakalo wajumuisha wapiganaji hao baada ya kuchujwa kwa makini.

Sanjari na hayo, mkataba huo unaitaka serikali ya rais Catherine Samba-Panza kutoa msamaha kwa ujumla, kusitisha muda wa mpito ambao kwa mujibu wa wajumbe hao umefika mwisho wake na kuunda taasisi za kiserikali zitakazokidhi matakwa ya wananchi, amesema mshiriki mmoja.

Hata hivyo, mapema mwezi huu, rais wa Congo-Brazzaville na msuluhishi wa mgogoro wa nchini Jamhuri ya Afrika ya kati, Denis Sassou-Nguesso, ameamua kuongeza muda wa miezi sita kwa mpito ambao ulitarajiwa kutamatishwa mwezi Februari.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.