Pata taarifa kuu
CAR-ANTIBALAKA-MATEKA-Usalama

Raia wa Ufaransa ashikiliwa mateka

Watu wawili, mmoja akiwa ni raia wa Ufaransa, ambao wote ni wafanyakazi katika shirika la kihisani la kitabibu la CODIS wametekwa nyara, Jumatatu Januari 19 asubuhi, mjini Bangui.

Mwanadini na raia moja wa Ufaransa wametekwa nyara wakati ambapo walikua wakisafiri kwa gari kaskazini mwa mji mkuu wa Jamhuri ya Afrika ya Kati.
Mwanadini na raia moja wa Ufaransa wametekwa nyara wakati ambapo walikua wakisafiri kwa gari kaskazini mwa mji mkuu wa Jamhuri ya Afrika ya Kati. AFP PHOTO / PACOME PABANDJI
Matangazo ya kibiashara

Mazungumzo yameanzishwa ili kujaribu kuwaachilia huru. Watekaji nyara ni wanamgambo wa Anti-balaka walio karibu na jenerali Andjilo, ambaye ni kiongozi wa kundi hilo, aliyekamatwa Jumamosi katika kijiji cha Bouca.

Wanamgambo hao wanadai kuachiliwa kwa kiongozi huyo wa kivita, ambaye alikamatwa na kikosi cha wanajeshi wa Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, Minusca.

Wafanyakazi hao walitekwa nyara wakiwa wanatokea katika kijiji kiliyo kwenye barabara inayoelekea Damara.

Kabla ya kuwasili katika kata ya Gobongo, watu wanne wenye silaha walisimama mbele ya gari na kumlazimisha dereva kusimama.

Mmoja ya watawa waliokua ndani ya gari hilo, aliachiliwa papo hapo, lakini watu hao wanne wenye silaha waliondoka na raia huyo wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 67 pamoja na mwanadini mengine, wakielekea katika kitongoji cha Boy-Rabe, mjini Bangui, ambapo ni ngome ya kundi la anti-balaka.

Viongozi wa Jamhuri ya Afrika ya Kati pamoja na Ufaransa wanajaribu kuelewa sababu ya kutekwa kwa watu hao. Inaonekana kwamba watekaji nyara ni wafuasi wa kiongozi wa kivita wa Anti-balaka, Andjilo.

Andjilo anatafutwa na vyombo vya sheria, akituhumiwa kutekeleza mauaji katika mji mkuu wa Jamhuri ya Afrika ya Kati, Bangui. Andjilo alikua aliukimbia mji wa Bangui, lakini alikamatwa Jumamosi iliyopita na kikosi cha wanajeshi wa Umoja wa Mataifa Minusca.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.