Pata taarifa kuu
SENEGAL-WADE-HAKI-SHERIA

Karim Wade agoma kula

Karim Wade, Waziri wa zamani, akiwa pia mtoto wa rais wa zamani wa Senegal, Abdoulaye Wade, ameanza mgomo wa kususia kula, kama alivyotangaza mwenyewe, Alhamisi Januari 15, wakati alipokua akisikilizwa katika Mahakama inayoshughulikia kesi za kujitajirisha kinyume cha sheria.

Karim Wade akiwasili mahakamani mjiniDakar, Julai 30 mwaka 2014.
Karim Wade akiwasili mahakamani mjiniDakar, Julai 30 mwaka 2014. AFP/PHOTO / STRINGER
Matangazo ya kibiashara

Karim Wade anatuhumiwa kwa muda sasa wa miezi sita kutumia vibaya madaraka yake kwa kujitajirisha kinyume cha sheria wakati alipokua Waziri katika utawala wa baba yake. Uamuzi huu wa Karim Wade unafuatia hali ya sintofahamu iliyotokea mnamo siku hizi mbili wakati kesi yake ilipokua ikisikilizwa.

Karim Wade alianza mgomo wa kususia kula ili kuonyesha kuwa kesi inayomkabili haiwezi kuendelea kusikilizwa kutokana na kukosekana kwa mawakili wake wakati ambao haki zake hazizingatiwi.

Mmoja kati ya wanasheria wa Karim Wade, Amadou Sall, alifukuzwa Mahakamani, baada ya kuhamakiana na jaji mkuu aliye kuwa akisimamia keshi hiyo. hatua hiyo ya kumfukuza Amadou Sall, ilisababisha wanasheria wake wote kuondoka kama ishara ya kupinga uamzi wa jaiji mkuu.

Sababu nyingine iliyopelekea Karim Wade kuchukua hatua hiyo, kitendo cha polisi cha kumdondosha chini akiwa kizimbani wakati alikua akifungwa pingu mikononi.

"Karim wade hapewi muda wa kupanga vizuri utetezi wake na kesi iliendelea kusikilizwa jana Alhamisi Januari 15 bila kuwepo mwanasheria hata mmoja, hali hii inaonyesha kuwa Karim wade hatendewi haki", amesema mwanaharakati mmoja wa haki za binadamu.

Waziri wa Sheria, Sidiki Kaba, ameutaka kila upande kuwa na utulivu. Kesi itasikilizwa tena Jumatatu Januari 19.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.