Pata taarifa kuu

Kukamatwa kwa Dominic Ongwen: taarifa zatafautiana

Baada ya tangazo la kukamatwa kwa Dominic Ongwen, mmoja wa viongozi wa juu katika kundi la waasi wa Uganda la LRA nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, taarifa za kukamatwa kwa kiongozi huyo zimekua zikitafautiana.

Picha ya zamani ya Dominic Ongwen baada yakuchapishwa kwenye mtandao wa polisi ya kimataifa ya Interpol.
Picha ya zamani ya Dominic Ongwen baada yakuchapishwa kwenye mtandao wa polisi ya kimataifa ya Interpol. AFP PHOTO / INTERPOL
Matangazo ya kibiashara

Dominic Ongwen yuko mikononi mwa kikosi maalumu cha wanajeshi wa Marekani na anazuiliwa katika eneo la Obo kusini mashariki mwa Jamhuri ya Afrika ya Kati, kwa mujibu wa chanzo cha kijeshi cha Uganda.

Lakini wapiganaji wa kundi la zamani la waasi la Seleka wamebaini kwamba, kiongozi huyo, ambaye ni mshirika wa karibu wa Joseph Kony, hakujisalimisha. Alikamatwa kufuatia mapigano.

Wapiganaji hao wa kundi la zamani la waasi la Seleka , wamethibitisha kwamba walimkamata Dominic Ongwen Januari 3 mwaka 2015 pembezoni mwa kitongoji cha Samoaja wakati wa mapigano, ambayo kwa mujibu wa duru hizo, yaligharimu vifo vya watu swatatu upande wa LRA.

Vikosi vya Marekani vilikua vilisambaza picha ya Ongwen, jambo ambalo lilipelekea kiongozi wa juu wa kundi la zamani la waasi la Seleka, Djouma Alanta, kumtambua kiurahisi. Akihojiwa na RFI, Djouma Alanta, amebaini kwamba aliwa taarifa wanajeshi wa Marekani siku 3 baada ya kukamatwa kwa Ongwen. Taarifa hii imethibitshwa na mkuu kijiji, alikokamatwa Ongwen.

Waasi wa zamani wa Seleka wameelezea masikitiko yao kuona Marekani haikutambua mchango wake kwa kumkamata na kumkabidhi moja wa viongozi wa juu wa LRA na washirika wa karibu wa Joseph Kony, ambaye pia ni mmoja kati ya viongozi wanne wa LRA wanaosakwa na Mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita ICC.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.