Pata taarifa kuu
KENYA-MGOMO-ELIMU

Mgomo wa waalimu Kenya

Walimu nchini Kenya leo Jumatatu Januari 5 wanatarajiwa kuanza mgomo katika nchi nzima kushinikiza serikali kutekeleza madai yao ya nyongeza ya mshahara pamoja na marupurupu mengine ambayo wanaidai.

Maandamano mbele ya Bunge, mjini Nairobi,Mei 14 mwaka 2013, dhidi ya kuongezwa mshahara kwa Wabunge.
Maandamano mbele ya Bunge, mjini Nairobi,Mei 14 mwaka 2013, dhidi ya kuongezwa mshahara kwa Wabunge. REUTERS/Thomas Mukoya
Matangazo ya kibiashara

Mgomo huo umeitishwa na chama cha Umoja wa Waalimu KNUT pamoja na KUPPET ambapo viongozi wake waliwataka wanachama wao kutoripoti kazini kuanzia siku ya Jumatatu ya tarahe 5 Januari mwaka 2015.

Chama cha wazazi nchini Kenya kimewasilisha kesi mahakamani kutaka kuzuiwa mgomo huo, uamuzi uliotangazwa na katibu mkuu wake Musau Ndunda ambaye amesisitiza kutofumbia macho mgomo huu.

Kwa upande wake, katibu mkuu wa KUPET, Akelo Missori, ametupilia mbali madai ya chama cha wazazi na kuongeza kuwa hawatishwi na amri iliyotolewa na Mahakama kuwataka kusitisha kwa muda mgomo huu.

Haya yanajiri wakati huu wazazi nchini Kenya wakiendelea kuwaandaa watoto wao kwa ajili ya kuanza mwaka mpya wa masomo 2015, huku pia kukiwa hakuna matumaini ya kufanyika kwa mazungumzo mengine kati ya waalimu na Serikali.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.