Pata taarifa kuu
DRC-FDLR-Usalama

Waasi wa kihutu wa Rwanda FDLR wajisalimisha

Sherehe za kuwapokonya silaha waasi wa Kihutu wa Rwanda FDLR zimefanyika Jumapili Desemba 28 katika mikoa ya Kivu ya Kaskazini na Kivu ya Kusini, nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Waasi wa Kihutu wa Rwanda (FDLR)wakijisalimisha na kurejesha silaha katika mji wa Kateku mashariki mwa Congo, Mei 30 mwaka 2014, chini ya usimamizi wa vikosi vya Umoja wa mataifa Monusco.
Waasi wa Kihutu wa Rwanda (FDLR)wakijisalimisha na kurejesha silaha katika mji wa Kateku mashariki mwa Congo, Mei 30 mwaka 2014, chini ya usimamizi wa vikosi vya Umoja wa mataifa Monusco. REUTERS/Kenny Katombe
Matangazo ya kibiashara

FDLR wakati huu iko chini ya shinikizo. Jumuiya ya kimataifa, hasa Shirikisho la kimataifa la nchi za kanda ya maziwa makuu (ICGLR) lilikua limetoa muda hadi Januari 2 waasi hao wa kihutu wa Rwanda wawe wamerejesha silaha kwa hiari yao, kabla hawajapokonywa kwa nguvu.

Lakini kwa mujibu wa viongozi, idadi ya silaha ziliyorejeshwa Jumapili Desemba 28 ni ndogo ikilinganishwa na idadi ya silaha zinazomilikiwa na waasi hao.

Wapiganaji 1400 wa kundi la waasi wa kihutu wa Rwanda ndio wanatakiwa kupokonywa silaha. Idadi hiyo imetolewa na viongozi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Wakati hayo yakijiri, Mbunge wa zamani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Vano Kiboko, wa jimbo la Katanga amezuiwa kuondoka nchini humo Jumapili Desemba 28 na Idara ya Uhamiaji katika uwanja wa ndege wa Ndjili mjini Kinshasa na kunyanganywa hati yake ya kusafiria akielekea mjini Paris na Marekani. Mke wake na watoto waliruhusiwa kuingia ndani ya ndege.

Hakuna maelezo yaliotolewa kuhusu kukataliwa Mbunge huyo kuondoka nchini. Akihojiwa na RFI, Vano Kiboko amebaini kuwa anaamini huenda ni maneno aliyotamka Jumamosi Desemba 27 wakati wa mkutano na waandishi wa habari ndio yamezua hali hiyo.

Katika mkutano nawaandishi wa habari, Vano Kiboko alisema kuwa chama tawala pamoja na vyama vinavyo unga mkono utawala vitalazimika kumteua mtu ambaye atagombea kwenye nafasi ya rais Joseph Kabila katika uchaguzi ujao wa rais na kuunga mkono uteuzi wa Moise Katumbi Chapwe, mkuu wa mkoa wa sasa wa Katanga.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.