Pata taarifa kuu
SIERRA LEONE-EBOLA-Afya

Muda wa kukabiliana na Ebola watamatika

Muda wa siku tano uliyowekwa na serikali ilikuzuiwa mambukizi ya virusi vya Ebola umemalizika Jumapili Desemba 28, kaskazini mwa Sierra Leone, nchi ambayo imeathirika zaidi na ugonjwa wa Ebola.

Licha ya hatua kadhaa za kukabiliana na Ebola, visa vipya vimekua vikigunduliwa nchini Sierra Leone.
Licha ya hatua kadhaa za kukabiliana na Ebola, visa vipya vimekua vikigunduliwa nchini Sierra Leone. REUTERS/Baz Ratner
Matangazo ya kibiashara

Hii ni mara ya pili Sierra Leone kuchukua hatua kama hiyo. Kwa muda wa siku tano, watu hawakuwa na haki ya kujielekeza madukani, kukusanyika au kutumia usafiri wa umma.

Sierra Leone iliorodhesha zaidi ya kesi 9,200 ya wagonjwa wa Ebola na hatua ziliyochukuliwa awali ili kukabiliana na ugonjwa huo hazikufaulu. Edward Conteh, mkazi wa mji wa Freetown amebaini kuwa hatua hizo hazikuleta mafanikio yoyote kwa kudhibiti ugonjwa wa Ebola.

Kila asubuhi jambo la kwanza anafanya ni kusoma katika gazeti takwimu za karibuni zinazotokana na mambukizi ya virusi vya Ebola.

 

Afrika bado inaendelea kujaribu kudhibiti mripuko wa Ebola, ambayo imesababisha zaidi ya watu 7,000 kufariki. Umoja wa Afrika ulikosolewa kushindwa kukabiliana na mripuko huo, na hadi leo, taasisi hiyo imeshindwa kutoa fedha ili kupambana dhidi ya ugonjwa huo.

Wiki iliyopita, Kituo cha Kimataifa kwa ajili ya mambo ya kimkakati kiliweza kupendekeza vitengo vyake kukusanya fedha, lakini pia kilianzisha teknolojia mbili muhimu ambazo huenda zikatekelezwa haraka iwezekanavyo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.