Pata taarifa kuu
ALGERIA-UFARANSA-Utekaji nyara

Mtu aliyehusika na kifo cha Hervé Gourdel auawa

Jeshi la Algeria limetangaza rasmi kuwauwa wanajihadi waatatu wanaotuhumiwa kuhusika na kifo cha mateka wa Ufaransa Hervé Gourdel.

Picha ya mateka wa Ufaransa Hervé Gourdel aliyeuawa Algeria.
Picha ya mateka wa Ufaransa Hervé Gourdel aliyeuawa Algeria. REUTERS/Patrice Massante
Matangazo ya kibiashara

Mapema asubuhi Jumanne Desemba 23 taarifa hii imerushwa kwenye vyombo vya habari kadhaa nchini Algeria, ambavyo vimethibitisha kwamba kiongozi wa kundi la kijihadi la Jund al-Khalifa, Abdelmalek Gouri, amefariki.

Abdelmalik Gouri ambaye anajulikana kwa jina halisi la Khaled Abou Souleimane, alihusika katika kitendo cha kumteka nyara na kumuua mateka wa Ufaransa Hervé Gourdel mwezi Septemba mwaka 2014.

Taarifa hii imethibitishwa rasmi asubuhi Jumanne Desemba mwaka 2014 na jeshi la Algeria. Abdelmalek Gouri huenda amefariki. Abdelmalik Gouri alikuwa kiongozi wa Jund al-Khalifa, kundi lililojiengua kwa kundi la Aqmi lenye mafungamano na kundi la Al-Qaeda, ambalo lilitangaza hivi karibuni kujiunga na kundi la wapiganaji wa Dola la Kiislam.

Mwezi Septemba, Abdelmalik Gouri alitangaza kumteka nyara, na siku chache baadae kumuua raia wa Ufaransa Hervé Gourdel. Kitendo ambacho kilitekelezwa kwa kulipiza kisasi, kwa mujibu wa kundi hilo la Jund al-Khalifa, kufuatia mashambulizi ya jeshi la Ufaransa dhidi ya kundi la wapiganaji wa Dola la Kiislam nchini Iraq.

Vyombo vya habari kadhaa vimekua vimetangaza Jumanne asubuhi kwamba Abdelmalek Gouri aliuawa pamoja na wanajihadi wengine wawili usiku wa Jumatatu kuamkia Jumanne, karibu na mji wa Algiers. Jeshi limebaini kwamba operesheni ilifanyika katika kitongoji cha Isser, katika eneo la Boumerdes, kilomita 60 mashariki ya mji mkuu Algiers.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.