Pata taarifa kuu
SENEGAL-AFRIKA-MKUTANO-USALAMA-AMANI

Mkutano wa Dakar watamatika kwa mafanikio

Baada ya siku mbili za mjadala katika mji mkuu wa Senegal, Dakar, mkutano wa kwanza wa kimataifa kuhusu amani na usalama barani Afrika umemalizika Jumanne Desemba 16. Ufaransa ilishirikiana na Senegal kwa kuundaa mkutano huo, jambo ambalo limeukera Umoja wa Afrika.

Mkutano wa kwanza wa kimataifa kuhusu amani na usalama barani Afrika, Dakar, senegal, Desemba 16 mwaka 2014.
Mkutano wa kwanza wa kimataifa kuhusu amani na usalama barani Afrika, Dakar, senegal, Desemba 16 mwaka 2014. AFP PHOTO / SEYLLOU
Matangazo ya kibiashara

Viongozi mbalimbali walioshiriki mkutano huo, wamebaini kwamba mkutano huo ulitoa nafasi ya mazungumzo yenye kujenga na kuleta maendeleo Afrika.

Hata hivyo suala la ugaidi nchini Libya limetawala mkutano huo, ambapo marais na viongozi wa serikali wametaka kuwepo na mbinu za pamoja kwa kuzuia kusambaa kwa makundi ya kigaidi barani Afrika.

Kwa mujibu wa waandaaji wa mkutano huo, mkutano wa Dakar umeleta mafaniko makubwa. Kwa upande wake, Waziri wa ulinzi wa Ufaransa, Jean-Yves Le Drian, amesema mkutano huo umepelekea wadau wote barani Afrika kukubaliana kuendelea na mazungumzo ya amani kila baada ya mwaka.

Katika mkutano huo baadhi ya mataifa ya Afrika yamelaumiwa kulipa fidia kwa makundi ya kigaidi yanapowashikilia watu mateka. Baadha ya viongozi wa Afrika wameona kuwa hali hiyo inaendelea kuyapa nguvu makundi ya kigaidi.

Marais wa Afrika wameiomba Ufaransa kupatia ufumbuzi suala la mdororo wa usalama nchini Libya, huku baadi ya marais hao hususan rais wa Chad, Idris Deby, kuyalaumu mataifa ya Magharibi kwamba ndiyo yalisababisha hali hiyo kutokea, baada tu ya kumuua rais wa nchi hiyo Moamar kadhafi. Kauli hiyo ya Idris Deby ilionekana kumuudhi Waziri wa Ufaransa Jean-Yves Le Drian.

“ Bwana Waziri utanisamehe kuona nimesema ukweli, lakini ni kwa marafiki zetu nchi mataifa ya Magharibi kutafutia suluhu katika nchi hiyo", amesema Idris Deby, huku akimshika mkono Waziri wa ulinzi wa Ufaransa, Jean-Yves Le Drian.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.