Pata taarifa kuu
AFRIKA KUSINI-PISTORIUS-Sheria

Kesi ya Pistorius: Mahakama yatazamiwa kutoa uamzi

Mahakama Afrika Kusini inatarajiwa Jumatano Desemba 10 kuamua ikiwa viongozi wa Mashtaka wanaweza kukata rufaa kwa kifungo cha miaka 5 alichopewa Oscar Pistorius kwa kumuua bila kukusudia mpenzi wake Reeeva Steenkamp.

Siku ya mwisho ya kusikilizwa kesi ya Oscar Pistorius, ambapo Mwendesha mashataka, Gerrie Nel, aliomba kifungo cha miaka 10 dhidi ya mwanariadha huyo mlemavu, Oktoba 17 mwaka 2014.
Siku ya mwisho ya kusikilizwa kesi ya Oscar Pistorius, ambapo Mwendesha mashataka, Gerrie Nel, aliomba kifungo cha miaka 10 dhidi ya mwanariadha huyo mlemavu, Oktoba 17 mwaka 2014. REUTERS/Werner Beukes/Pool
Matangazo ya kibiashara

Oscar Pistorius alipewa hukumu hiyo mwezi Oktoba baada ya kupatikana na kosa hilo la mauaji bila kukusudia.

Oscar Pistorius aisabahi familia yake kabla ya kupelekwa jela, Oktoba 21 mwaka 2014.
Oscar Pistorius aisabahi familia yake kabla ya kupelekwa jela, Oktoba 21 mwaka 2014. REUTERS/Herman Verwey/Pool

Viongozi wa Mashtaka walionesha kutoridishwa kwao na hukumu aliyopewa Pistorius na kusema watakata rufaa ili mwanaridha huyo Mlemavu apewe kifungo kikali zaidi.

Mbali na kifungo hicho cha miaka mitano, viongozi hao wa Mashtaka wanataka kukata rufaa pia kupinga kwa kosa la mauji bila kukusudia na kumshtaki kwa kosa la kuua kwa kukusudia.

Viongozi wa Mashtaka wakiongozwa na Gerrie Nel wanataka Pistorius apewe kifungo cha miaka 15 kwa kuua kwa kukusudia.

Jaji Thokozile Masipe aliyetoa hukumu dhidi ya Pistorius ndiye atakayetoa hukumu Jumatano Desemba 10 ikiwa viongozi wa Mashtaka wakate rufaa au la.

Viongozi wa Mashtaka wanasema, Jaji Masipa alitafsiri visivyo sheria kuhusu mauaji na kesi hiyo inastahili kuendelea katika Mahakama ya rufaa.
 

Mwanariadha wazamani wa Afrika Kusini Oscar Pistorius.
Mwanariadha wazamani wa Afrika Kusini Oscar Pistorius. REUTERS/Siphiwe Sibeko

Hadi uamuzi huo utakapotolewa, Pistorius anaendelea kukitumia kifingo cha miaka mitano jela katika jela ya KGOSI Mampuru.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.