Pata taarifa kuu
SENEGAL-UFARANSA-FRANCOPHONIE

Afrika yapoteza nafasi katika uongozi wa OIF

Michaëlle Jean amepitishwa Jumapili Novemba 30 mjini Dakar, nchini Senegal, kuwa katibu mkuu wa Jumuiya ya Kimataifa ya nchi zinazozungumza Kifaransa (OIF). Raia huyo wa Canada mwenye asili ya Haiti anachukua nafasi ya Abdou Diouf, rais wa zamani wa Senegal.

Rais wa Ufaransa, François Hollande, akimpongeza Michaëlle Jean, baada ya kupitishwa kwenye uongozi wa OIF.
Rais wa Ufaransa, François Hollande, akimpongeza Michaëlle Jean, baada ya kupitishwa kwenye uongozi wa OIF. AFP PHOTO / SOW MOUSSA
Matangazo ya kibiashara

Ni kwa mara ya kwanza mwanamke na raia asiyetokea Afrika kushikilia nafasi hiyo. Mkutano wa kilele wa mwaka huu umekua na mageuzi makubwa.

Michaëlle Jean atakabidhiwa rasmi madaraka ya uongozi wa Jumuiya hiyo, Januari 1 mwaka 2015.

Michaëlle Jean, mwenye umri wa miaka 57, na ambaye aliwahi kuwa mwandishi wa habari, ni mwanamke wa kwanza kushikilia nafasi hiyo kwenye Jumuiya ya Kimataifa ya nchi zinazozungumza Kifaransa. Michaëlle Jean, ambaye ni mjukuu wa raia mweusi mtumwa hakuwa anasita kukemea biashara ya watumwa ambayo ilifanywa kwa muda mrefu katika bandari ya Ufaransa.

Ni kwa mara ya kwanza bara la Afrika kutoongoza Jumuiya ya Kimataifa ya nchi zinazozungumza Kifaransa. Zoezi la kumchagua rais mpya wa Jumuiya ya Kimataifa ya nchi zinazozungumza Kifaransa ambalo limefanyika katika faragha katika dakika za mwisho nchini Senegal, limezua utata. Wakati huohuo rais wa Cote d'Ivoire Alassane Ouattara aliamua kuondoka katika mkutano huo.

OIF imetoka mikononi mwa bara la Afrika. Kwa kipindi cha miaka 4 OIF itakua chini ya uongozi wa bara la Amerika ya Kaskazini. Hali hiyo huenda ikasababisha ushirikiano kudorora kati ya Ufaransa na baadhi ya nchi za Afrka zinazozungumza Kifaransa.

Michaëlle Jean, amepitishwa kwenye uongozi wa Jumuiya hiyo, kwa sababu mbalimbali. Kwanza kwa sababu ni mwanamke, na ni kwa mara ya kwanza mwanamke anashikiliwa nafasi hiyo. Na sababu nyingine, ni mtu ambaye anatokea Amerika ya Kaskazini.

Zoezi la kumchagua katibu mkuu wa Jumuiya hiyo liligubikwa na mvutano kati ya wajumbe waliyoshiriki mkutano huo hadi kupelekea kura kupigwa. Mwishoe, ilibidi wachukuliwe viongozi sita wa nchi na serikali zilizokua na wagombea katika uchaguzi huo, ikiwa ni pamoja na Denis Sassou-Nguesso rais wa Congo-Brazzavile, Waziri mkuu wa canada Stephen Harper, rais wa Ufaransa François Hollande, rais wa Senegal Macky Sall, rais Pierre Nkurunziza wa Burundi pamoja na rais wa Mauritania Kailash Purryag, ambao wamekutana katika faragha kwa muda wa saa moja ili wafikie makubaliano kuhusu nani atapitishwa kuongoza Jumuiya ya Kimataifa ya nchi zinazozungumza Kifaransa.

Itafahamika kwamba Michaëlle Jean amepitishwa baada ya Afrika kushindwa kuelewana kuhusu nani anayepaswa kumrithi Abdou Diouf kwenye nafasi ya katibu mkuu wa Jumuiya ya Kimataifa ya nchi zinazozungumza Kifaransa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.