Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 26/03 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 26/03 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 26/03 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Afrika

Burkina Faso: mvutano waibuka kuhusu marekebisho ya katiba ya mpito

media Zéphirin Diabré, kiongozi wa upinzani, mbele ya vyombo vya habari, baada ya mkutano na wawakilishi wa vyama vya kiraia, viongozi wa kidini na kimila, Ougadougou, Novemba 11 mwaka 2014. ISSOUF SANOGO / AFP

Hali ya kutokukubaliana imeanza kujitokeza nchini Burkina Faso baina ya viongozi wa kijeshi na wadau wengine baada ya jeshi hilo chini ya Luteni Kanili Isaac Zida kufanya marekebisho ya rasimu ya mkataba.

Viongozi wa kijeshi nchini Burkina Faso wamemkabidhi Jumanne Novemba 11 rais wa Senegal Macky Sall, aliyekuja na rais wa Togo, Faure Gnassingbé kwa niaba ya ECOWAS, marekebisho yao kwa rasimu ya mpito ya mkataba uliyoafikiwa na vyama vya siasa vya upinzani mapoja na vyama vya kiraia.

Zida amependekeza kupunguzwa kwa kiasi kikubwa kwa idadi yamihimili ya serikali ikiwa ni pamoja na Bunge la mpito, baraza la ulinzi na usalama na tume ya taifa ya maridhiano, msimamo ambao rais wa Senegal Macky Sall anakubaliana nao kwa muda huu wa mpito.

 

Siku kumi baada ya kutimuliwa madarakani rais wa zamani Blaise Compaoré, upinzani na vyama vya kiraia walilikabishi jeshi Jumatatu Novemba 10 rasimu ya mkataba wa mpito. Rasimu hio ya mkataba ya mpito inapendekeza kuundwa kwa taasisi mbalimbali za uongozi wa nchi, hususan, uteuzi wa rais asiye kuwa jeshi aidha polisi, kuundwa kwa serikali yenye mawaziri 25 pamoja na Bunge lenye wajumbe 90. Jeshi lilipendekeza marekebisho ya rasimu hiyo, ambayo yaliwasilishwa kwa vyama vya upinzani, vyama vya kiraia , viongozi wa kidini na kimila.

Marekebisho hayo yaliibua hisia tofauti kati ya upinzani na vyama vya kiraia. Upinzani uko tayari kujadili marekebisho hayo, na ulipanga kuanza zoezi hilo Jumatano Novemba 12 asubuhi.

Vyama vya kiraia, hata hivyo, itakuwa vigumu kuviashawishi. "Binafsi, siungi mkono marekebisho hayo yaliyofanywa na jeshi," amesema mwanasheria Luc Marius Ibriga, wakati wajumbe wengine wamefikia hadi kulani " jaribio la mapinduzi" ya kijeshi.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana