Pata taarifa kuu
DRC-BENI-ADF-M23-Usalama

DRC: waasi wa zamani wa M23 waishushia lawama serikali ya Congo

Waasi wa zamani wa M 23 waliofurushwa na serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo pamoja na wanajeshi wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani, wameituhumu serikali ya Congo kutokua na nia ya kutekeleza makubaliano waliyoafikia mjini Nairobi, nchini Kenya.

Bertrand Bisimwa, aliye kuwa kiongozi wa waasi wa zamani wa M23, Bunagana, Machi 7 mwaka 2013.
Bertrand Bisimwa, aliye kuwa kiongozi wa waasi wa zamani wa M23, Bunagana, Machi 7 mwaka 2013. Photo AFP / Isaac Kasamani
Matangazo ya kibiashara

Makubaliano hayo ya amani yalifikiwa jijini Nairobi nchini Kenya mwaka mmoja uliopita kati ya waasi wa M23 na serikali ya Congo.

Kiongozi wa waasi hao wa zamani, Betrand Bisimwa ameimbai Idhaa ya Kiswahili ya RFI kuwa hawaamini kuwa serikali ya Congo itatekeleza mwafaka huo ambao ni pamoja na kuwahakikishia usalama wao ikiwa watarudi nchini humo kama ilivyokubaliwa.

Aidha, Bisimwa amelaani mauaji yanayotekelezwa na waasi wa ADF-Nalu mjini Beni na kuikashifu serikali kwa kushindwa kuwapa usalama raia wake na kukanusha madai kuwa wanahusika kwa namna moja au nyingine na mauaji hayo.

Hata hivyo, mashirika ya kiraia Mashariki mwa nchi hiyo bado yanaamini kuwa, waasi hao wa zamani bado wana mkono kuhusu ukosefu wa usalama katika Wilaya ya Beni.

Mji wa Beni na vitongoji vyake vimekua vikishambuliwa na watu wenye silaha, ambao hadi sasa bado hawajajulikana. Hata hivyo serikali ya congo imekua ikinyooshea kidole kundi la waasi wa uganda la ADF-Nalu, ikibaini kwamba kundi hilo limekua likiendesha harakati zake mashariki mwa Congo.

Baadhi ya vyama vya upinzani vimekua vikiomba uchunguzi uanzishwe ili kujua watu wanaoendesha mauaji ya raia wasiokua na hatia katika maeneo hayo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.