Pata taarifa kuu
AFRIKA KUSINI-PISTORIUS-Sheria

Kesi ya Pistorius: Mwendesha mashitaka akata rufaa

Ofisi ya Mwendesha mashtaka nchini Afrika Kusini imekata rufaa ya hukumu ilyotolewa dhidi ya mwanariadha wa zamani Oscar Pistorius. Barua ya kukata rufaa imewasilishwa rasmi Jumanne Novemba 4, baada ya Pistorius kuhukumia septemba 12 kwa kosa la kuua bila kukusudia.

Oscar Pistorius alihukumiwa kifungo cha miaka mitano jela Septemba 12 mwaka 2014.
Oscar Pistorius alihukumiwa kifungo cha miaka mitano jela Septemba 12 mwaka 2014. REUTERS/Siphiwe Sibeko
Matangazo ya kibiashara

Msemaji wa Ofisi ya mashitaka katika ngazi ya kitaifa nchini Afrika Kusini, Nathi Mncube, ametangaza kuwa Ofisi hiyo imekataa rufaa dhidi ya hukumu na dhidi ya tuhuma ambazo zilibadilishwa, baada ya Ofisi ya mashtaka kumtuhumu Oscar Pistorius kwamba alimuua mpezi wake kwa kukusudia.

Baada ya hukumu dhidi ya Oscar Pistorius kutolea afisa wa Ofisi ya mashitaka alifahamisha kwamba Pistorius hangelipaswa kupewa hukumu ya kifungo cha miaka mitano.

Wakati kesi ya Pistorius ilipokua ikisikilizwa afisa wa Ofisi ya mashitaka iliomba mahakama imuhukumu Pistorius kifungo cha miaka kumi jela. Lakini majaji walimuhukumu mwanariadha huyo kifungo cha miaka mitano jela wakibaini kwamba upande wa mashtaka haukutoa vithibitisho tosha.

Mwanariadha huyo, mwenye umri wa miaka 27, yuko jela mjini Pretoria, baada ya kuhukumiwa kifungo cha miaka mitano jela septemba 12.

Kesi ya Pistorius iliyodumu miezi minane ilizua mvutano nchini Afrika Kusini. Hata hivyo Ofisi ya mashitaka itasubiri jibu la jaji, ambaye ataruhusu au la rufaa hiyo, na kuna uwezekano kesi hiyo irudi kusikilizwa baada ya miezi sita.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.