Pata taarifa kuu
BURKINA FASO-Katiba-Siasa

Burkina Faso: Zida yuko tayari kukabidhi madaraka kwa raia

Luteni kanali Yacouba Isaac Zida aliye pitishwa na jeshi kuchukua mamlaka ya uongozi wa nchi, baada ya kujiuzulu kwa Blaise Compaoré, amesema Jumanne Novemba 4 kwamba yuko tayari “kukabidhi madaraka ya uongozi wa nchi kwa raia”.

Luteni kanali Isaac Zida, Ouagadougou Novemba 2 mwaka 2014.
Luteni kanali Isaac Zida, Ouagadougou Novemba 2 mwaka 2014. AFP PHOTO / ISSOUF SANOGO
Matangazo ya kibiashara

“ Wamekuja kutuambia kwamba watakabidhi madaraka kwa raia. Tumepongeza uamzi huo, na tumewataka wafanye hivyo kwa manufaa ya taifa”, amesema Mogho Naba mkuu wa jamii kuu nchini Burkina Faso, ambaye anaheshimiwa nchini humo.

Kiongozi huyo amempokea kwa mazunguzo luteni kanali Yacouba Isaac Zida akishirikiana na ujumbe wa wa wanajeshi.

Luteni kanali Isaac Zida, hakusema lolote kuhusu ziara hiyo, bali baada ya mazungumzo na kiongozi huyo aliingia ndani ya gari lake nyeusi kabla ya kuondoka, na walinzi wake. Afisa huyo wa jeshi anatazamiwa kukutana kwa mazungumzo na rais wa Baraza la Katiba.

Tangu mwanzoni wa mgogoro huo, Luteni Kanali Isaac Zida amekua akijizuia na kauli ambazo zinaweza kuchochea machafuko nchini Burkina Faso. Jumatatu Novemba 3, alisema kwamba serikali itaongozwa na taasisi ya mpito ambayo itateuliwa kulingana na mfumo wa kikatiba" na rais wa mpito atateuliwa kwa makubaliano ya wadau wote ".

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.