Pata taarifa kuu
BURKINA FASO-Katiba-Siasa

Burkina Faso: Zida aahidi kuunda serikali kwa mfumo wa kikatiba

Hatma ya Burkina Faso haijulikane, baada ya hali ya wasiwasi kutokea Jumapili Novemba 2, ambapo mamia kwa maelfu ya vijana waliandamana mbele ya majengo ya televisheni ya serikali. Mtu mmoja aliuawa katika maandamano hayo.

Luteni kanali Yakouba Isaac Zida aliye pitishwa na jeshi kwenye mamlaka ya uongozi wa nchi akiwa pamoja na Zephirin Diabre, mmoja kati ya viongozi wa upinzani, Jumapili Novemba 2 mwaka 2014.
Luteni kanali Yakouba Isaac Zida aliye pitishwa na jeshi kwenye mamlaka ya uongozi wa nchi akiwa pamoja na Zephirin Diabre, mmoja kati ya viongozi wa upinzani, Jumapili Novemba 2 mwaka 2014. REUTERS/Joe Penney
Matangazo ya kibiashara

Jeshi limebaini kwamba litaendelea na majukumu yake ya kulinda taifa licha ya kuwa linaendelea kukabiliwa na changamoto ya waandamanaji lakini pia kuendelea na mazungumzo na upinzani na vyama vya kiraia.

Luteni kanali Yacouba Isaac Zida, ameahidi kuunda serikali ya mpito kulingana na jinsi Katiba inavyoeleza. Hata hivo hali ya utulivu imeripotiwa Jumatatu Novemba 2 katika mji mkuu wa Burkina Faso, Ouagadougou.

Shuguli zimerudi kuendeshwa kama kawaida. Shule na duka zimefunguliwa. Amri ya kutotoka nje imepunguzwa na kusogezwa mbele. Raia wametakiwa kutotoka nje tangu usiku wa manane hadi saa 11 alfajiri. Mipaka ya nchi imefunguliwa, lakini safari za ndege hazijaanza huenda viwanja vya ndege vikafunguliwa hivi karibuni.

Luteni kanali yacouba Isaac Zida, amekutana kwa mazungumzo na mabalozi wanaowakilisha nchi zao nchini Burkina Faso. Hayo yanajiri wakati viongozi wa upinzani wanapanga kukutana Jumatatu mchana Novemba 3 kwenye makao makuu ya chama cha kiongozi wa upinzani, Zéphirin Diabré.

Kwa upande wake kundi la usuluhishi wa kimataifa linaloundwa na Umoja wa Mataifa, Umoja wa Afrika na Jumuiya ya maendeleo ya nchi za Afrika ya Magharibi (Cedeao) limetishia kuwachukulia vikwazo viongozi wa kijeshi iwapo Katiba haitoheshimishwa. Katiba inaeleza kuwa Spika wa Bunge ndiye anapaaswa kuchukua mamlaka ya uongozi wa nchi, iwapo rais atakua hashikilii tena madaraka hayo kwa sababu mbalimbali.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.