Pata taarifa kuu
BURKINA FASO-Katiba-Siasa

Burkina Faso: Hali ya wasiwasi yaendelea kutanda Ouagadougou

Mazungumzo kwa minajili ya kuunda serikali ya mpito yanaendelea nchini Burkina Faso, wakati ambapo hali ya wasiwasi ikiendelea kushuhudiwa katika baadhi ya maeneo ya nchi, hususan katika mji wa ouagadougou.

Yacouba Isaac Zida akikutana kwa mazungumzo na wawakilishi wa upinzani nchini Burkina Faso, Novemba 2 mwaka 2014, mjini Ouagadougou.
Yacouba Isaac Zida akikutana kwa mazungumzo na wawakilishi wa upinzani nchini Burkina Faso, Novemba 2 mwaka 2014, mjini Ouagadougou. REUTERS/Joe Penney
Matangazo ya kibiashara

Mtu mmoja alifariki Jumapili Novemba 2 wakati vijana walikua wakiandamana wakijaribu kuingia katika majengo ya televisheni ya taifa. Hali bado ni tete nchini Burkina Faso. Hata hivo Yacouba Isaac Zida aliye pitishwa na jeshi kwa kushikilia mamlaka ya uongozi wa nchi anaendelea kukutana na wadau wote katika hali ya kutafutia ufumbuzi maandamano yanayoendelea.

Jumapili Novemba 2 watu wawili mmoja akiwa afisa wa jeshi na mwengine raia wa kawaida walijitangaza kila mmoja akidai kua ni rais wa Burkina Faso. Vikosi vya usalama vililazimika Jumapili Novemba 2 kufyatua risase hewani ili kuwatawanya waandamanaji ambao walikua wakijaribu kuingia katika majengo ya televisheni ya taifa kumuunga mkono mmoja kati ya wanasiasa wa upinzani, Saran Sérémé ili aweze kujitangaza rais wa Burkina Faso.

Hali hiyo katika mji wa Ouagadougou ambayo ilisababisha kifo cha mtu mmoja inatokea wakati mvutano umeendelea kujitokeza kuhusu uundwaji wa serikali ya mpito. Katika mkutano na waandishi wa habari, msemaji wa Yacouba Isaac Zida, amewatahadhari raia ambao watajaribu kuingia barabarani.

Hayo yanajiri wakati yacouba Isaac Zida amekutana Jumapili alaasiri Novemba 2 na ujumbe wa wanasiasa wa upinzani. Mazungumzo yao yalifanyika katika mazingira mazuri, bila kuwepo na mvutano. Afisa huyo wa jeshi amekutana pia na mabalozi wa mataifa ya madharibi wanaowakilisha nchi zao nchini Burkina Faso, hususan balozi wa Marekani, wa Ufaransa pamoja na mwakilishi wa Umoja wa Ulaya. Mabalozi hao wameunga mkono shinikizo la Umoja wa Afrika ambao umependekeza kuwa mamlaka ya uongozi wa nchi upewe raia wa kawaida, licha ya kuwa jambo hilo sio rahisi.

Katika jitihada za kuunda serikali ya mpito, Yacouba Isaac Zida amekutana kwa mazungumzo na aliye kuwa rais wa Burkina Faso, Jean-Baptiste Ouédraogo. Rais huyo wa zamani aliwatolea wito raia kuwa watulivu na kusubiri matokeo ya mazungumzo kati ya jeshi na wadau wote katika suala zima la ujenzi wa Burkina Faso.

Ninatolea wito raia, muachane na mambo ambayo yataendelea kusababisha chuki kati yenu. Tujihusishe na maendeleo ya taifa kuliko kuendeleza vurugu”, amesema Jean-Baptiste Ouédraogo.

 

Jumapili Novemba 2, tume ya mseto iliyojumuisha Umoja wa Mataifa, Umoja wa Afrika na Jumuiya ya maendeleo ya Afrika ya magharibi ( Cédéao) imekutana na wadau wote husika katika mgogoro unaoendelea Burkina Faso tangu kujiuzulu kwa Blaise Compaoré. Tume hiyo imeomba pande zote kuheshimu katiba ya nchi na kulitaka jeshi kukabidhi raia mamlaka ya uongozi wa nchi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.