Pata taarifa kuu
BURKINA FASO-Katiba-Siasa

Burkina Faso: mkutano kati ya jeshi na wanasiasa

Hali ya wasiwasi imeendelea kushuhudiwa katika mji mkuu wa Burkina Faso Ouagadougou, ambapo umati wa watu umejaribu Jumapili Novemba 2 kuingia katika majengo ya televisheni ya serikali ORTB.

Luteni kanali Isaac Zida, Ouagadougoi, Novemba 1 mwaka 2014.
Luteni kanali Isaac Zida, Ouagadougoi, Novemba 1 mwaka 2014. REUTERS/Joe Penney
Matangazo ya kibiashara

Wakati huohuo wanajeshi waliokua kwenye ulinzi waliwatawanya watu hao kwa kufyatua risase hewani. Awali, jenerali mstaafu Kouamé lougué alionekana kwenye televisheni akijitangaza kuwa ni rais, wakati ambapo mwanasiasa wa upinzani, Saran Sérémé, amekataliwa kutoa taarifa yoyote kwenye vyombo vya habari.

Luteni Kanali Zida, ambaye alipitishwa jumamosi Novemba 1 na jeshi kuliongoza taifa la Burkina Faso, amekutana jumapili Novemba 2 na ujumbe wa wanasiasa.

Wakati majadiliano yakiendelea mjini Ouagadougou kati ya jeshi na wanasiasa, hali ya utulivu imerejea katika mji huo baada ya machafuko kutokea pembezuni mwa redio, ambapo watu wawili walijitangza kwa muda unaopisahana dakika tatu kuwa ni marais wa Burkina Faso.

Umati wa watu umekua umekusanyika mbele ya majengo ya televisheni mapema jumapili asubuhi Novemba 2 mwaka 2014, kabla ya kutawanywa na vikosi vya usalama ambavyo vilijaribu kufyatua risase hewani. Waandamanaji wengine ambao wamekua wameandaa maandamano katika eneo la taifa walitawanywa pia na vikosi hivyo vya usalama.

Mkutano kati ya Luteni Kanali Zida na wawakilishi wa wanasiasa umefanyika katika makao makuu ya Baraza la Uchumi na Jamii (CES) mjini Ouagadougou, shirika la habari Burkina24. Baada ya kukutana na waandishi wa habari, Isaac Zida, ambaye amepewa mamlaka na jeshi ya kuliongoza taifa la Burkiana Faso alirejea ukumbini kukutana na ujumbe mkubwa wa wanasiasa, hususuan wa upinzani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.