Pata taarifa kuu
TOGO-Uchaguzi-Siasa

Togo: Kanisa zahamasisha raia kudai mageuzi

Maaskofu na wachungaji nchini Togo wamewataka wanasiasa kurejelea mchakato wa mazungumzo wakati wa mkutano uliofanyika Oktoba 1 mwaka 2014 mjini Lomé. Upinzani na utawala hawajaafikiana kuhusu mageuzi ambayo yanatakiwa kufanyika kwenye Katiba ya nchi, hususan suala la mihula ya rais.

Askofu Nicodème Barrigah, Mwenyekiti wa Tume ya ukweli, sheria na maridhiano nchini Togo.
Askofu Nicodème Barrigah, Mwenyekiti wa Tume ya ukweli, sheria na maridhiano nchini Togo. cvjr.org/
Matangazo ya kibiashara

Kwa muda wa miaka minane sasa mvutano ulikua bado ukiendelea kati ya utawala na upinzani. Upinzani unaomba kuweko na nia madhubuti yake na serikali kwa kuzingatia maslahi ya taifa.

Katika wito huo wa pamoja uliyosainiwa na naibu kiongozi wa Baraza kuu la maaskofu nchini Togo, wawakilishi wa Kanisa za kiinjili na madhehebu mengine nchini Togo wameelezea kushangazwa na msimamo wa Bunge la Togo la kutupilia mbali uwezekano wa kuidhinisha mswada wa Katiba ya taifa hilo.

Mkataba wa kisiasa uliyosaniwa kati ya utawala na upinzani mwaka 2006, unaomba kuweko na mageuzi ya kikatiba yatakayo ridhiwa na makundi yote kwa lengo la kudumisha mchakato wa kuendeleza demokrasia.

Katika mageuzi hayo kuna kuweka kikomo kwenye mihula ambayo rais anatakiwa kuwa madarakani na kuandaa awamu mbili wakati wa uchaguzi wa rais, jambo ambalo halijafanyika tangu kufanyike marekebisho ya Katiba Desemba mwaka 2002. kwa mujibu wa viongozi hao wa kidini walioweka saini zao kwenye waraka huo, ni jambo ambalo halieleweki, na linakuja kudhorotesha makubaliano yaliyoafikiwa na wanasiasa.

Viongozi hao wa kidini wameelezea masikitiko yao kuona baada ya Bunge kutupilia mbali mswada huo wa marekebisho ya Katiba, hakuna jambo lilichofanyika ili kupatia ufumbuzi suala hilo muhimu kwa hatma ya taifa la Togo. Maskofu na wachungaji hao wamemtolea wito rais wa Jamhuri, serikali, Spika wa Bunge na upinzani kuandaa mageuzi kwenye Bunge la taifa hilo kwa minajili ya kuondoa kasoro ambayo inaweza kujitokeza kwa wakati wowote katika uchaguzi wa rais unatazamiwa kufanyika mwaka 2016.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.