Pata taarifa kuu
UFARANSA - ALGERIA - USALAMA

Wahusika wa mauaji ya Herve Gourdel watambulika

Takriban juma moja baada ya kutokea kwa  mauaji ya Herve Gourdel raia wa Ufaransa, huko nchini Algeria, viongozi wa serikali ya Algeria, wamethibitisha kuwatambua wahusika wa mauaji hayo yaliotekelezwa baada ya kumteka nyara.

picha ya Herve Gourdel katika eneo la Saint-Martin-Vesubie, September 25, 2014.
picha ya Herve Gourdel katika eneo la Saint-Martin-Vesubie, September 25, 2014. Reuters/路透社
Matangazo ya kibiashara

Waziri wa sheria nchini humo Tayeb Louh ndiye ambaye ametowa taarifa hii, kundi linalo itwa jeshi la Califat ndilo lililohusika baada ya kuthibitisha hilo kupitia mkanda wa video iliochapishwa jana siku ya jumatatu juma lililopita. Hapo jana septemba 30 mkanda mwingine wa video ulichapishwa kwenye mitandao ya Internet.

Mkanda huo wa video ambao hauna tarehe, na wenye dakika takriban nne, imechapishwa kwenye mtandao wa youtube jana jioni. Katika mnada huo unaofanana na picha za video zinazochapishwa na kundi la islamic State, zinaonekana picha za ramani ya Afrika, bunduki aina ya kalachinikov na kitabu kitakatifu Quran pamoja na bendera ya kunsi la Islamic State.

Watu zaidi ya thalathini ambao wanaoshukiwa kuwa wanajeshi wa Califat, kundi ambalo limekiri kutekeleza mauaji ya raia huyo wa Ufaransa Herve Gourdel wameonekana wakisimama wima wengine wakichutama na wote wakionekana kubebelea silaha aina ya AK47 lakini pia silaha nzito nzito hususan silaha inayo tumiwa kwa kurusha roketi.

Katika sehemu ya kwanza Abou Abdallah el- Assimi anaongea. Alikuwa muasisi wa kundi la kigaidi nchini Algeria la GSPC, ambalo baadae mwaka 2007 liligeuka na kuwa kundi la Alqeda katika ukanda wa maghreb la Aqmi. Abdelmalek Gouri mwenye umri wa miaka 37 anaonekana pia kwenye mkandsa huo mwenye asili ya Alger mchungaji zamani. Huyo pia alijiunga katika kundi la GIA, Groupe Islamique Arme, kabla ya kujiunga na kundi la GSPC na baadae kujiunga na kundi la Aqmi.

Kundi hili limekuwa hatari sana na linajihusisha na ulipuaji wa mabomu ya kujitowa muhanga nchini Algeria tangu kipindi kadhaa. Mahakamaya Algeria iliwahi kumuhukumi kifungo cha maisha jela bila ya yeye kuwepo mahakamani.

Waziri wa sheria wa algeria Tayeb Louh amefahamisha kuwa vyombo vya usalama nchini humo, vimefaulu kuwatambuwa wengi miongoni mwa wanaharakati wa kundi hilo. Hii ndio kauli ya kwanza rasmi kutolewa na viongozi wa nchi hiyo tangu kutokea kifo cha Herve Gourdel. Uchunguzi umekabidhiwa jaji wa mahakama ya Alger mtaalamu wa maswala ya ugaidi na mauaji yakupangwa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.