Pata taarifa kuu
Cote d'Ivoire - ICC

Charles Blé Goudé wa tawi la vijana katika utawala wa Laurent Gbagbo afikishwa kizimbani

Charles Blé Goudé kiongozi wa zamani wa tawi la chama tawala nchini Côte d’Ivoire anafikishwa kizimbani hii leo kwenye mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita ya ICC ilopo mjini Hege nchini Uholanzi. Kiongozi huyo alifikishwa katika mahakama hiyo mwezi March iliopita na anatuhumiwa makosa ya uhalifu wa kivita katika virugu zilizoibuka baada ya uchaguzi mkuu wa rais wa mwaka 2010-2011. Hadi alhamisi hii atakuwa tayari ametambua hatma yake

Charles Ble Goude kiongozi wa zamani wa tawi la vijana katika utawala wa Laurent Gbagbo
Charles Ble Goude kiongozi wa zamani wa tawi la vijana katika utawala wa Laurent Gbagbo
Matangazo ya kibiashara

Kwa takriban muda wa siku nne kititi, korti kuu ya mahakama hiyo ya kimataifa itajaribu kuweka bayana iwapo kiongozi huyo wa tawi la vijana katika chama tawala zamani nchini Côte d’Ivoire ana kosa la kujibu au la.

Kulingana na muendesha mashtaka, kiongozi huyo anawajibika katika mauaji, ubakaji na mateso. Mauaji yaliotekelezwa kati ya desemba 16 mwaka 2010 na Aorul 12 mwaka 2011. Anatuhumiwa kuajiri vijana na kuwapa silaha vijana waliokuwa wakimuunga mkono Laurent Gbagbo baada ya uchaguzi mkuu wa Novemba 2010.

Kwa kipindi cha siku nne, watetezi wanatakiwa kupinga tuhuma dhidi ya mteja wao na kuwasilisha viashiria kwamba hajahusika kwa njia yoyte ile. Huenda Charles Blé Goudé akasikika katika utetezi wake kwa kipindi hiki.

Baraza la utangulizi litakuwa na siku 60 kutowa uamuzi wake, kuamuwa iwapo kiongozi huyo anakesi ya kujibu au la, iwapo mashtaka yaliowasilishwa ni pungufu hayatoshi kesi hiyo kuskilizwa. Wakati akiwasilishwa katika mahakama hiyo ya ICC mwezi March iliopita, kiongozi huyo wa vijana wa FPI alisema haogopi kufikishwa mahakamani kwakuwa anaimani kwamba hana haitia na atarejea nchini mwake baada ya kusafishwa.

Mahakama hiyo ilitangaza hivi karibuni kwamba kesi ya rais wa zamani wa cote d'Ivoire Laurent Gbagbo ambaye pia anashikiliwa katika mahakama hiyo ya Hegue itasikilizwa pia kwenye mahakama hiyo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.