Pata taarifa kuu
MISRI

Hukumu mpya dhidi ya Hosni Mubarak kutolewa

Siku ya Jumamosi jijini Cairo nchini Misri, Mahakama itatoa hukumu mpya dhidi ya rais wa zamani Hosni Mubarak kwa tuhma za ufisaidi na mauaji ya waandamanaji wakati wa maandamano ya wananchi dhidi ya uongozi wake mwaka 2011.

Hosni Mubarak akiwa Mahakamani mwaka 2013
Hosni Mubarak akiwa Mahakamani mwaka 2013 REUTERS/Stringer/Files
Matangazo ya kibiashara

Mubarak mwenye umri wa miaka 86, amekuwa akizuiliwa pamoja na watoto wake wawili wa kiume na Waziri wa zamani wa Mambo ya ndani.

Wanawe, Alaa na Gamal wote wanakitumikia kufungo cha miaka minne jela kwa kosa la utumizi mbaya wa fedha za umma wakati wa uongozi wa babake.

Hosni Mubarak
Hosni Mubarak

Mubarak naye alitozwa faini ya Dola Milioni 3 na kuagizwa kulipa Dola Milioni 17 nukta 6 kwa tuhma za kuiba fedha za wananchi na pia kuhukumiwa jela miaka mingine mitatu.

Awali, Mubarak alipatikana na hatia mwaka 2012 na kuhukumiwa kifungo cha maisha jela, lakini baadaye Mahakama ilibadilisha hukumu hiyo.

Wafuasi wa Hosni Mubarak
Wafuasi wa Hosni Mubarak REUTERS/Youssef Boudlal

Wachambuzi wa Mambo wanasema Mubarak ambaye aliongoza Misri miaka 30 kabla ya kuondolewa na wananchi huenda akaachiliwa huru baada ya baadhi ya mashahidi kubadilisha ushahidi wao.

Mwezi uliopita rais huo wa zamani aliiambai Mahakama kuwa alipokuwa rais, alijitahidi kadiri ya uwezo wake kutetea haki za binadamu nchini humo na kuitetea nchi ya Misri dhidi ya maadui wake.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.