Pata taarifa kuu
UFARANSA-ALGERIA-Utekaji nyara

Algeria: Jitihada za kumtafuta mateka wa Ufaransa zaendelea

Ufaransa imetupilia mbali onyo liliyolewa na watekaji nyara wa raia wa Ufaransa Hervé Gourdel na kubaini kwamba itaendelea na mashambulizi dhidi ya wapiganaji wa Dola la Kiislam nchini Iraq.

Kikosi cha wanajeshi wa Algeria wakitafuta mateaka wa Ufaransa, Septemba 23 mwaka 2104.
Kikosi cha wanajeshi wa Algeria wakitafuta mateaka wa Ufaransa, Septemba 23 mwaka 2104. REUTERS/Louafi Larbi
Matangazo ya kibiashara

Raia huyo wa Ufaransa alitekwa nyara jumapili Septemba 21 katika eneo la Tizi Ouzou, karibu kilomita 110 mashariki mwa mji mkuu wa Algeria, Algiers. Jeshi la Algeria limeongeza juhudi ya kumtafuta mateka huyo katika eneo la milima mashariki mwa Algiers ili kujaribu kujua wapi anakoshikiliwa mateka huyo ambaye anakabiliwa na kitisho cha kuuawa.

Takriban kikosi cha wanajeshi 2000 wanaedelea na jitihada za kumtafuta mateka huyo, huku wakizunguuka eneo la milima la Djurdjura katika mji wa Kabylie, ambapo raia huyo wa Ufaransa alitekwa nyara.

Kwa mujibu wa vyanzo vya usalama, kundi hilo la watekaji nyara lilikua linaundwa na watu sita.

Wakati huo huo Wizara ya Ulinzi ya Ufaransa ilifahamisha jumanne alaasiri wiki hii kwamba ilimuua gaidi mmoja katika jimbo huo aliko tekwa nyara Hervé Gourdel, bila hata hivo kubaini kwamba mtu huyo alikua na uhusiano na watekaji nyara hao. Hata hivo serikali ya Algeria kupitia Waziri wa Mambo ya Nje, Abdelkader Messahel, ilibaini kwamba haitotii kamwe madai ya magaidi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.