Pata taarifa kuu
LIBERIA-SIERRA LEONE-Afya-Ebola

Ebola imeendelea kuzua hali ya wasiwasi Afrika ya magharibi

Hali ya wasiwasi imeendelea kutanda katika nchi zinazokumbwa na Homa ya Ebola. Maelfu ya visa vya ugonjwa huo vinasubiriwa nchini Liberia mnamo wiki tatu zijazo, Shirika la Afya Duniani (WHO), limeonya.

Katika kijiji cha Kailahun, nchini Sierra Leone, watu waliojitolea wakifanya mazishi ya mtu aliefariki kutokana na ugonjwa wa Ebola, 18 Julai mwaka 2014.
Katika kijiji cha Kailahun, nchini Sierra Leone, watu waliojitolea wakifanya mazishi ya mtu aliefariki kutokana na ugonjwa wa Ebola, 18 Julai mwaka 2014. REUTERS/WHO/Tarik Jasarevic
Matangazo ya kibiashara

Shirika la Afya Duniani limesema kumekua na ongezeko la maambukizi ya ugonjwa wa Ebola katika mataifa kunakoshuhudiwa ugonjwa huo, hususan nchini Liberia na Sierra Leone, wakati ambapo watu 2000 wamefariki kutokana na ugonjwa wa Ebola.

Hata hivo Umoja wa Afrika kama mashirika mengine ya kimataifa na kikanda, umetoa wito wa kuondoa marufuku ya kusafiri katika mataifa yanayokumbwa na ugonjwa wa Ebola kwa kuhofia kueneza katika mataifa ambayo hayajaathiri.

Hayo yakijiri, mtu mmoja aneaminika kuambulizwa ugonjwa wa Ebola Afrika ya magharibi atasafirishwa nchini Marekani, ambako atawekwa karantini, viongozi wa hospitali iliyo karibu na mji wa Atlanta kusini mashariki mwa Marekani wamefahamisha, bila hata hivo kubaini jina la mtu huyo na uraia wake.

“Mgonjwa huyo anatazamiwa kuwasili mjini Atlanta jumanne wiki hii, lakini haijafahamika saa akayofikia”, vyanzo vya hospitali vimeeleza.

Hospitali hii, iliwahudumia kimatibabu daktari mmoja, raia wa Marekani, Kent Brantly, aliye ambukizwa virusi vya Ebola pamoja na msaidizi wake, Nancy Writebol. Watu hao waliruhusiwa hivi karibuni kuondoka hospitali, baada ya kupona ugonjwa huo.

Hayo yakiarifiwa, daktari mwengine wa Shirika la Afya Duniani (WHO), ameamukizwa virusi vya Ebola nchini Sierra Leone, na anatazamiwa kusafirishwa, WHO imetangaza jumatatu wiki hii.

Kwa mara ya kwanza virusi vya Ebola viligundulika mwaka 1976 mskariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.