Pata taarifa kuu
RWANDA-RDF-Usalama

Rwanda: maafisa wastaafu wanaendelea kukamatwa

Jeshi la Rwanda limethibitisha kumtia mbaroni afisa wake mstaafu mwingine, wa tatu baada ya jenereli Frank Rusagara na Capitaine David Kabuye kama sehemu ya uchunguzi kwa tuhuma za "uhalifu dhidi ya serikali" ya Kigali.

Jenerali Joseph Nzabamwita akiwa na wanajeshi wake katika jimbo la Busura, Novemba 4 mwaka 2012.
Jenerali Joseph Nzabamwita akiwa na wanajeshi wake katika jimbo la Busura, Novemba 4 mwaka 2012. AFP PHOTO / STEPHANIE AGLIETTI
Matangazo ya kibiashara

Akihojiwa na RFI, msemaji wa jeshi la Rwanda, Jenerali Joseph Nzabamwita amethibitisha kuwa kamanda mkuu wa zamani wa walinzi wa rais Kagame Kanali Tom Byabagamba amekamatwa miongoni mwa wanaotuhumiwa kwa uhalifu huo.

Hivi karibuni, Kanali Tom Byabagamba alirejea nchini Rwanda baada ya kushika nafasi ya juu katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini huku kukiwepo na hofu kuwa mke wa David Kabuye, mama Rose Kabuye na Mary Baine, mke wa Kanali Byabagamba huenda na wao pia wakatiwa mbaroni.

Mapema jumatatu wiki hii, msemaji mmoja wa wizara ya mambo ya nje ya Marekani ameiambia RFI kwamba nchi yake tayari imeiomba Rwanda kuheshimu taratibu za mchakato wa mahakama na kuweka wazi kwa umma mashtaka ya watuhumiwa hao, na kujibiwa na Jenerali Joseph Nzabamwita kuwa Rwanda ni taifa huru.
“Nchi ya Rwanda haihitaji ushauri kutoka kwa mtu yeyote”, amesema Nzabamwita.

Kulingana na mchambuzi mmoja wa Rwanda, kamatakamata hiyo inayoendeshwa nchini humo inawalenga hasa askari ambao wanaonekana kuutumia vilivyo uhuru wao ndani ya serikali ya Rwanda na kwa hiyo, kwa mujibu wa chanzo hicho, "Lengo ni kurejesha nidhamu katika safu ya chama tawala.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.