Pata taarifa kuu
AFRIKA KUSINI-Siasa

Afrika Kusini: Jacob Zuma ahojiwa na wabunge

Polisi wa kutuliza ghasia nchini Afrika Kusini, siku ya Alhamisi walilazimika kuimarisha usalama kwenye ukumbi wa bunge la nchi hiyo baada ya vikao vyake vya hapo jana kuvunjika kutokana na fujo zilizoibuliwa toka kwa wabunge waliokuwa wakimzomea rais Jackob Zuma wakati akijibu maswali.

Rais wa Afrika Kusini, Jacob Zuma, ahojiwa na wabunge.
Rais wa Afrika Kusini, Jacob Zuma, ahojiwa na wabunge. (Photo : Reuters)
Matangazo ya kibiashara

Vurugu ndani ya bunge hilo zilizuka wakati rais Zuma alipokuwa akihojiwa kuhusu matumizi ya kiasi cha dola milioni 24 pesa za walipa kodi wa nchi hizo zilizotumika kuboresha makazi yake.

Wabunge hao wa upinzani wakiongozwa na mwenyekiti wa chama cha Economic Freedom Fighters, Julius Malema alikaidi agizo la spika wa bunge Baleka Mbete kuwataka watoke nje ya ukumbi huo na badala yake walianza kupiga kelele za kumtaka rais Zuma kurejesha fedha hizo.

Baada ya vurugu hizo, spika aliomba msaada toka kwa vyombo vya usalama ambapo wabunge wa chama tawala walilazimika kutoka nje wakati polisi hao wakiwadhibiti wabunge wa EFF.

Wabunge wa EFF wamekuwa changamoto kwa bunge la nchi hiyo kwa aina ya mavazi ya Overall na yawahudumu wa hoteli ambayo wamekuwa wakiyavaa ndani ya bunge.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.