Pata taarifa kuu
MALI-AZAWAD-GATIA-Uasi-Usalama

Mali: Kundi jipya la Uasi lazuka kaskazini mwa Mali

Kundi jipya la watu wenye silaha kutoka jamii ya Watuareg limezuka kaskazini mwa Mali. Kundi hilo ambalo limebaini kwamba lengo lake ni kujihami dhidi ya watu ambao wana malengo ya kuligawa taifa la Mali, limepiga kambi karibu na mji mkuu wa Mali, Bamako.

Kundi jipya la watu wenye silaha liliyozuka nchini Mali lina uhusiano na Alaji Gamou ( kwenye picha), afisa katika ngazi ya juu wa jeshi la Mali kutoka jamii ya watuareg.
Kundi jipya la watu wenye silaha liliyozuka nchini Mali lina uhusiano na Alaji Gamou ( kwenye picha), afisa katika ngazi ya juu wa jeshi la Mali kutoka jamii ya watuareg. RFI/Moussa Kaka
Matangazo ya kibiashara

Waanzilishi wa kundi hilo wamesema kwamba wanapinga mapango wa kuligawa taifa la Mali, hususan kaskazini mwa taifa hilo ambako makundi ya waasi yanashikilia.

Kundi hilo jipya la uasi linaundwa na watu wa jamii ya watuareg kutoka kabila la Imrad, ambao wanapatikana katika mikoa mitatu ya Mali. Kundi hilo la watu wa jamii ya watuareg kutoka kabila la Imrad na washirika wake (Gatia) wamedai kuwa na maelfu ya wapiganaji.

Waasi hao wamethibitisha kwamba kambi yao inapatikana kati ya mji wa Gao na Kidal. Hata hivo haijabainika iwapo kundi hilo na washirika wake wamechukua silaha dhidi ya serikali ya Mali. Lakini wamebaini kwamba hawatokubali taifa la Mali liwe na bendera mbili, na hali hiyo ndiyo imepelekea wachukuwe silaha dhidi ya makundi ambayo yana malengo ya kuligawa taifa hilo.

Kundi lenye ushirikiano wa karibu na Alaji Gamou

Katibu mkuu wa kundi la waasi la Gatia linalo shirikiana na kundi hilo jipya la watu wa Jamii ya watuareg, Fahad Ag Almahmoud, ana matumaini ya kushiriki katika mazungumzo ya kusaka amani yanayotazamiwa kufanyika katika mji mkuu wa Ageria, Algiers. Fahad Ag Almahmoud, ameweka wazi ukweli wake kwamba kundi lake lina ushirikiano wa karibu na Alaji Gamou, afisa wa ngazi ya juu katika jeshi la Mali, mwenye cheo cha ujenerali, ambaye ni kutoka jamii ya watuareg. Kundi la Azawad (MAA), ambalo linaungwa mkono na serikali ya Mali ni mshirika pia wa karibu wa kundi hilo jipya liliyozuka nchini Mali.

Hata hivo kundi la waasi la Gatia halijawa tayari kuketi pamoja na kundi la Azawadi ambalo limekua gumzo kwenye vyombo vya habari.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.