Pata taarifa kuu
MISRI-HRW-Haki za binadamu

Misri : HRW : Mauaji ya wafuasi wa Mohamed Morsi yalipangwa

Shirika la kimataifa la Haki za Binadamu, Human Right Watch limetoa ripoti ya kurasa 188, ambamo linatuhumu jeshi la Misri kutekeleza mauaji ya wafuasi zaidi ya 700 wa rais Mohamed Morsi, aliye timuliwa madarakani na jeshi liliyokua likiongozwa na Abdel Fattah al-Sissi.

Mamia kwa maelfu ya wafuasi wa rais Mohamed Morsi wakiandamana wakipinga uamzi wa jeshi wa kuondoa mamlakani kiongozi wao.
Mamia kwa maelfu ya wafuasi wa rais Mohamed Morsi wakiandamana wakipinga uamzi wa jeshi wa kuondoa mamlakani kiongozi wao. REUTERS/Mohamed Abd El Ghany
Matangazo ya kibiashara

Wafuasi wa Mohamed Morsi wakiandamana mbele ya makao makuu ya jeshi.
Wafuasi wa Mohamed Morsi wakiandamana mbele ya makao makuu ya jeshi. REUTERS/Khaled Abdullah

Human Right Watch imebaini kwamba mauaji hayo yalilenga wafuasi wa Mohamed Morsi ambao walikua wakipinga kutimuliwa kwa kiongozi huyo, na kusema kwamba mauaji hayo yulipangwa kuanzia ngazi ya juu ya kijeshi.

Humana Right Watch imesema jeshi la Misri lilitekeleza uhalifu dhidi ya binadamu.

Agosti 14 mwaka 2013, mwezi moja baada ya kiongozi wa majeshi ya Misri Abdel Fattah al-Sissi kumuondoa madarakani rais aliyechaguliwa Mohamed Morsi, ilidhihirika wazi kwamba wafuasi wa rais Morsi ndio walikua wakilengwa, baada ya mamia ya wafuasi wa kiongozi huyo kuuawa katikati ya mji wa Cairo.
Le gouvernement a reconnu la mort, ce jour-là, de plus de 700 manifestants.

Katika ripoti hiyo iliyooneshwa mjini Cairo kwa njia ya video kutokea mjini New York nchini Marekani, HWR imetaja mashuhuda 200, walioshuhudia mauaji ya watu 817 katika eneo pekee la Rabba, huku wakinyooshea kidole jeshi la Misri kuhusika na vifo hivyo, baada ya wafuasi hao kuandamana dhidi ya hatua iliyotangazawa na kiongozi wa jeshi, Abdel Fattah al Sissi ya kumtimua mamlakani Mohamed Morsi, Julai 3 mwaka 2013.

“katika eneo pekee la Rabba, jeshi la Misri lilitekeleza mauaji makubwa dhidi ya wafuasi zaidi ya 300 kwa siku mchana mmoja”, amesema mkurugenzi mtendaji wa HRW, Kenneth Roth, ambaye Jumapili wiki iliyopita serikali ya Misri ilikataa kumruhusu kuingia nchini Misri, ambapo alikua anatazamiwa kutoa ripoti hiyo.

Rais wa Misri, Abdel Fattah al-Sissi, ambaye anatuhumiwa na HRW kuhusika na mauwaji ya zaidi ya 1000 ya wafuasi wa Mohamed Morsi.
Rais wa Misri, Abdel Fattah al-Sissi, ambaye anatuhumiwa na HRW kuhusika na mauwaji ya zaidi ya 1000 ya wafuasi wa Mohamed Morsi. REUTERS/The Egyptian Presidency/Handout

HRW imewataja maafisa wa ngazi ya juu jeshini na katika polisi, viongozi wa kisiasa, akiwemo rais wa sasa Abdel Fattah al-Sissi,ambaye wakati huo alikua waziri wa ulinzi pamoja na waziri wa mambo ya ndani, Mohamed Ibrahim. HRW imesema watu hao wanapaswa kufanyiwa uchunguzi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.